Home » Articles » COMPUTER

NAHITAJI KUWA NA TOVUTI (WEBSITE) YANGU MWENYEWE NIFANYEJE?

NAHITAJI KUWA NA TOVUTI (WEBSITE) YANGU MWENYEWE NIFANYEJE?


Inawezekana kuwa hili ni swali ambalo unalitafutia jibu siku zote. Umeona website nyingi sana zikiwa na maudhui mbalimbali ambayo yamekuvutia. Nyingine zikiwa na rangi mbalimbali zenye mvuto. Lakini ni nani hasa anayemiliki website hizo? Au je na wewe unaweza kuwa na website yako? Fuatilia makala hii nawe upate ujuzi juu ya hili na pengine siku chache zijazo na wewe unaweza kuwa na ya kwako.

 

Kumbuka kwamba websites (tovuti) hazianzishwi tu hovyohovyo bila kuwa na malengo fulani. Mfano kwa lengo la kutoa elimu, kutangaza biashara, kurahisisha kazi za usajili katika taasisi mbalimbali au idara mbalimbali, kusambaza taarifa mbalimbali za kitaifa na kimataifa au hata kutoa matokeo ya mitihani iliyofanyika katika kiwango fulani cha elimu, pia wengine huanzisha tovuti zao kwa lengo la kujitangaza wao wenyewe hasahasa wakiwa ni wasanii au kundi fulani au hata chama fulani. Je wewe unataka kuanzisha website(tovuti) kwa lengo gani?

 

Hili ni swali ambalo la kwanza kabisa unapaswa kujiuliza kabla ya kuamua kutengeneza tovuti yako. Sasa umeshajua lengo la tovuti yako, kinachotakiwa sasa ni kujua jinsi gani uitengeneze hiyo website yako.

Website zinatengenezwa kutokana na wewe unavyohitaji iwe. Ndio maana websites hazifanani kila website ina muonekano wake tofauti na nyingine, hii ni kutokana na matakwa ya mwenye tovuti hiyo. Vile vile tovuti inatengenezwa kulingana na lengo lake kwa mfano tovuti zinazohusu elimu haziwezi kufanana na zile zinazohusu wasanii na burudani. Na hata kabla hujaisoma basi ule muonekano wake tu utakupelekea kutabiri lengo la website yako.

Unaweza kujiuliza je? Ni vipi sasa inatengenezwa?

Kwanza ni vema ujue mambo yafuatayo kabla ya kuendelea.

Kuna tovuti za bure ambazo tayari zimekwishatengenezwa, wewe kazi yako ni kujisajili na kuanza kujaza vitu vyako humo. Baada ya kujisajili unachotakiwa ni kuchagua aina ya muonekano wa tovuti na kisha uendelee na kujaza mambo mbalimbali. Lakini tovuti hizi zinakupa fursa ya kutengeneza anuani yako lakini baada ya anuani yako lazima ifuatiwe na anuani ya kwao kisha anuani nzima ikamilike kwa mfano. www.anuaniyako.anuaniyao.com  hii ina maana kwamba website yako umeitengeneza bure ndani ya website ya www.anuaniyao.com.

 

Kwa mfano kuna website inaitwa www.webs.com. Hii kila mtu anaweza kutengeneza website yake humu ila kama unahitaji website yako iitwe abc basi address yako kamili itakuwa www.abc.webs.com.

Baadhi ya wesite hizo kama unahitaji ni kama hizi:-

www.ucoz.com

www.simplesite.com

www.jigsy.com

www.wix.com

www.weebly.com

www.zoho.com

www.yola.com

www.jimdo.com

hivyo kama unahitaji njia rahisi ya kutengeneza website bila gharama yoyote basi jaribu kati ya hizo hapo.

Majina yote hayo hapo juu ndio kitaalamu yanajulikana kama Domain names. Na lile utakaloongeza wewe ili litambulike katika kufungulia website yako litakuwa ni Sub-domain. Kwa mfano umeamua kutumia www.ucoz.com ili wawe ndio free hoster wako hivyo kama unataka jina la "abc” liwe ndio address yako basi litakuwa www.abc.ucoz.com. Hapo "abc” ni Sub-domain na "ucoz” ndio Domain.

Lakini hizo zina vikwazo fulani fulani kama vile sio rahisi watu kutambua jina la kampuni yako kwani litakuwa limechanganyika katika jina la kampuni nyingine, pia hutaweza kutengeneza email kwa kutumia jina la kampuni yako kwa mfano someone@yourcompany.com. Vilevile search engine haitakupa kipaumbele katika matokeo pale mtu anapotafuta aidha katika google au Bing au hata search engine yeyote ile.

Hivyo kama unahitaji tu kwa sababu ndogondogo basi haina neno ukatumia njia hizo hapo juu, lakini kama unahitaji kuwa na website kubwa yenye malengo makubwa basi usitumie Sub-domains bali jitahidi usajili kwa malipo katika tovuti za Domain registrar ili uwe na Domain name yako mwenyewe kwa mfano www.yourname.com au kama ni jina tulilolitolea mfano hapo juu "abc” liwe www.abc.com basi na sio kuchanganyika na  jina jingine.

Kumbuka website zote hapo juu unaweza kusajili bure kisha ukajaza vitu katika website hiyo ya bure na baada ya kuona imekamilika, haohao wanatoa huduma ya kusajili Domain  name kwa malipo  (yanatofautiana katika kila website) hivyo baada ya kuwalipa website yako badala ya kupatikana kwa mfano www.abc.webs.com sasa inapatika kwa www.abc.com kwa muonekano uleule.

Zifuatazo ni website za kusajili ili uwe na Domain name yako mwenyewe kwa malipo ya mwaka mmoja au zaidi ukipenda.

www.onlydomains.com

www.godaddy.com

www.domains.ucoz.com

www.domainrightnow.com

www.1&1.com

www.namecheap.com

www.name.com

na nyinginezo. Hivyo basi hayo ni baadhi ya mambo au dondoo endapo unahitaji kuwa na website yako mwenyewe. Kumbuka wengine huita blog lakini kuna tofauti fulani kati ya blog na website Bofya hapa kujua tofauti hizo, lakini utaratibu wa kusajili blog ni kama huuhuu wa website.

Nashukuru kwa kuwa pamoja nami, endapo utakuwa na la zaida, swali, maoni, usisite kutoa hapa kwani tovuti hii ni yetu sote kwaajili ya kuelimishana sote na kila mwenye wazo zuri lenye manufaa katika jamii anakaribishwa kuchangia hapa. Ahsante.

Category: COMPUTER | Added by: Admin (26/Dec/2013) | Author: yahya Mohamed W
Views: 3332 | Tags: website, tengeneza, blog, Register, Domain, tafuta, mwenyewe, tovuti, Computer, sajili | Rating: 3.0/1
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: