Home » Articles » COMPUTER

NJIA RAHISI YA KUKUMBUKA PASSWORD YAKO KATIKA USER ACCOUNTS

"PASSWORD HINT”

NJIA RAHISI YA KUKUMBUKA PASSWORD YAKO KATIKA USER ACCOUNTS


Sote tunajua kuwa password ni neno lolote au mchanganyiko wa herufi pamoja na namba unaotumiwa na mwenye account kutumia account yake kwa usalama zaidi.

 

Katika windows unaweza kutengeneza neno lako la siri (password), ili kwamba ni wewe tu ndiye unayeweza kutumia kompyuta yako, na neno hilo ni wewe tu ndiye unalolifahamu na sio mwingine yeyote.

 

Kuna njia nyingi sana ambazo zimetengenezwa kukusaidia katika kukumbuka neno lako la siri endapo utakuwa umelisahau, hali ambayo inaweza kukupelekea kushindwa kutumia kompyuta yako mwenyewe. Katika windows kwenye user accounts njia ya kwanza na ya msingi ni kitu kinachoitwa "password hint” je? Password hint ni nini? Na jinsi gani unaweza kuitumia? Kuwa nami pamoja tuendelee kuelimishana juu ya hili.

 

Ni rahisi sana kutumia ila ni vema nikiwaonyesha nini maana yake, kwani watu wengi sana hutumia password hint vibaya hali ambayo hupelekea kutoweka kompyuta zao katika hali ya usalama au kutopata faida yoyote ya password hint.

 

Password hint ni neno lolote au sentensi inayoelezea maana halisi ya password au neno lako la siri, hivyo ni wazo zuri kuwa na password hint ili kuisaidia kumbukumbu yako. Password hint bora na yenye msaada zaidi kwako ni ile yenye maneno, sehemu ya neno au namba ambayo inaleta tafsiri fulani katika password au neno lako la siri.

 

 Mfano unaweza kuweka neno lako la siri kama "pilau” halafu ukatengeneza password hint kama "chakula anachokipenda dada yangu” hii inamaana kuwa huwezi kuingia na kutumia kompyuta yako mpaka ujaze neno pilau ndio ifunguke. Sasa endapo utasahau siku moja kuwa neno lako la siri ni pilau basi kuna chaguo litakuja ambalo litakuonyesha password hint yako ambayo ni "chakula anachokipenda dada yangu”. Hapo unaweza kukumbuka kuwa chakula anachokipenda dada yangu ni pilau hivyo tayari unakuwa umeshafaulu kuikumbuka password au neno lako la siri.

 

Na hiyo password hint hutokea mara tu unapokosea kujaza neno lako la siri kwa  mara ya kwanza kabisa.

 

Mfano wa jinsi password hints zinavyoweza kutengenezwa.

 

PASSWORD

PASSWORD HINT

JOHN

Jina la mjomba wangu nimpendae

+1600564326

Namba ya simu ya mke wangu

Nyoka

Mdudu atembeaye bila ya kuwa na miguu

ukimwi

Ugonjwa wa zinaa

 

Unatengeneza password hint pale unapotengeneza neno la siri au password mpya au unapolibadilisha.


Muhimu:

  1. Ni muhimu kujua kwamba mtu yeyote anayetumia kompyuta yako atakuwa na uwezo wa kuona Password hint pale tu atakapojaribu kubuni neno la siri ili aingie na kutumia kompyuta yako kisha akakosea kama tulivyokwisha eleza hapo awali. Hivyo basi hakikisha password hint yako inakuwa ngumu kwa mtu kubahatisha neno lako la siri.

 

Mfano wa baadhi ya password hint ambazo ni rahisi sana mtu kubahatisha ni kama zifuatazo:-

 

  1. Bara kubwa kabisa ulimwenguni ……. Mtu yeyote anaweza kubahatisha kuwa ni "asia
  2. Mdudu anayesambaza malaria…….. Mtu yeyote anaweza kubahatisha kuwa ni "mbu
  3. Sayari ya kwanza kutoka kwenye jua … Mtu yeyote anaweza kubahatisha kuwa ni "zebaki” au "Mercury

 

Na nyingine zinazofanana na hizo, hivyo usijitie katika mashaka kwa kuweka password hint rahisi kama hizo.

 

  1. Kuna baadhi ya watu ambao hawajapata elimu juu ya hili hujaza password hint kwa kutumia neno la siri au password ileile hali ambayo inapelekea kutokuwa salama katika matumizi yake ya kompyuta kwani password hint huonekana na kila mtu. Mfano neno la siri hujaza "computer” na password hint huweka hilohilo neno "computer” au

"kabati” na password hint huweka hilohilo neno "kabati”

Hivyo jitahidi kuwa makini juu ya hili.

 

  1. Tengeneza hint ambayo inaelezea maana ya password au neno lako la siri na usitumie hint ambayo haina faida yoyote. Mfano wa hint kama hizo ni:-

Neno la siri "Madagascar” na hint yake " chakula cha jioni” au neno la siri ni "John” na hint yake " Amerca” sasa tunaona ugumu hapa kuwa, Madagascar na chakula cha jioni havina uhusiano wowote ule au John na Amerca pia havina uhusiano wowote hivyo endapo utasahau neno lako la siri na kompyuta ikakuonyesha kuwa hint yako ni "Chakula cha jioni” basi kazi kubwa unayo kwani unaweza kujaza kama vile ndizi, mihogo, chapati n.k. hali ambayo inakugharimu sasa. Niliwahi kumshuhudia mtu anaweka password hint alama ya kituo yaani ".” Lakini nilipopeleleza nikagundua kuwa hakuelewa maana yake hivyo akaona kuliko kuacha sehemu ile wazi bila kujaza chochote ni bora aweke tu hiyo alama.

 

Nashukuru kwa kuwa pamoja nami na kusoma elimu hii ndogo ambayo naona huweza kuleta manufaa kwa watumiaji wengi wa computer na kurekebisha makosa yao madogo madogo. Tutaendelea kutoa mafunzo mbali mbali juu ya mambo kama haya ili tunufaike na elimu hii ya kompyuta.

 

Pia jisikie huru kutoa maoni yako hapa au kuchangia lolote juu ya mada hii ili watu wapate kunufaika zaidi. Na pia nakaribisha maswali yoyote kama unatatizo lolote na mashine yako (computer) ili niweze kukusaidia kwa kadiri ya ujuzi niliojaaliwa, kama una swali jisikie huru kuuliza kwa kubofya hapa na kuuliza swali lako.

 

Nadhani kwa kufikia hapa kuanzia leo utakuwa na ujuzi juu ya kuchagua password hint iliyosahihi na salama zaidi. Karibu tena katika tovuti hii ambayo imesheheni elimu mbalimbali pamoja na burudani tofauti na kukupa wewe mtembeleaji nafasi ya kuweka kile unachopenda kuchangia na wenzio. Nakutakia kila la kheri katika kutafuta kile bora unachohitaji.

 

Category: COMPUTER | Added by: Admin (13/Mar/2013)
Views: 3059 | Tags: komputer, neno la sri, password hint, kumbuka, password, Computer | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: