Home » Articles » COMPUTER

Tuumalize ubishi wa DVD V/S CD

Tuumalize ubishi wa DVD V/S CD


Hakuna asiyejua leo hii kuwa DVD ni kubwa kuliko CD kwani ina uwezo wa kuhifadhi taarifa nyingi kuliko CD na ndio maana hata bei yake kuwa juu zaidi ya CD, lakini hivi karibuni sehemu tofauti nimesikia juu ya ubishi kati ya CD na DVD. Ubishi huu ni kwamba mmoja anadai ya kwamba CD ni jina la ujumla linalomaanisha DVD na VCD, na mwingine akisema kuwa DVD inajitegemea na CD inajitegemea. Hebu tuangalie hapa usahihi ni upi.

Hebu tuangalie kwanza kirefu cha hayo maneno:

CD – Compact Disk

VCD – Video Compact Disk

DVD – Digital Video Disk

Tukiangalia majina yote hayo tunaona kuwa kuna neno "Disk” mwisho. Zimeitwa Disk kwa kuwa zina asili ya Duara (kisahani). Hata ile inayoitwa Hard Disk katika computer unaweza kujiuliza mbona imeitwa Disk lakini haiko duara? Ukweli ni kwamba ukiifungua ndani utaona kisahani cha rangi kama ya Gold ambacho kazi yake ni kuhifadhi taarifa zote zinazowekwa humo. Tutaangalia jinsi hard Disk inavyohifadhi taarifa katika makala ijayo.

Niliwahi kwenda duka moja kununua empty CD, nilipofika nikamwambia nahitaji CD empty, muuzaji akaniuliza unahitaji CD gani DVD au VCD? Ukweli ni kwamba DVD siyo CD ila tu kwa mazoea yetu tumejenga fikra kwamba kila Disk inaitwa CD hadi DVD pia. Sio mbaya ikiwa tutatumia uzoefu wetu huu kwani ndiyo njia rahisi ya kuelewana lakini tusiweke akilini kuwa CD ni neno la ujumla linalomaanisha Disk zote hadi DVD.

Ile disk yenye ukubwa wa Megabyte 650 hadi 700 ambayo ndiyo rahisi na inauzwa Tsh 500/= haiitwi VCD ikiwa tupu, hupewa jina la VCD pale tu itakaporekodiwa Video ndani yake. Ila ikiwa tupu huitwa CD (Compact Disk) hata kwa ushahidi nenda kanunue CD empty hiyo halafu isome, hutakuta hata siku moja ikiandikwa juu yake VCD bali itaandikwa CD – R or CD – RW au vinginevyo lakini neno CD lazima lianze.


Kama ingekuwa zinaitwa VCD basi ungenunua empty ingeandikwa VCD – R badala ya CD –R . lakini ile disk yenye ukubwa wa GB 4.7 huitwa DVD (Digital Video Disk) hata kama ikiwa empty, hilo ndilo jina lake na hata ukinunua tupu ambayo haijarekodiwa utaona juu imechapishwa DVD – R or DVD – RW. Hivyo basi fahamu ya kwamba kwa sasa tuna aina mbili ambazo ni CD na DVD hakuna VCD, VCD huitwa hivyo ikiwa imerekodiwa picha ndani yake. Kuna aina nyingine kama blue ray disk n.k lakini mada yetu haiko huko.


Sio mbaya tukiendelea kutumia uzoefu wetu wa mawasiliano katika kununua CD kwani kinachohitajika ni kuelewana tu, lakini kwa kutaka kufahamu kiundani na kuepusha ubishi watu wanapobishana juu ya suala hili basi makala hii itakusaidia kumuelewesha anayetaka kujua.

Kila siku tunajifunza hivyo tusichekane bali tueleweshane kwa upole, na kwa kufanya hivyo tutakuwa ni wenye ufahamu mzuri sana.

Kwa hapa sina la ziada labda ikiwa una la kuongeza au maoni, maswali na ushauri usisite kuwasiliana nasi. Nakutakia kila la kheri katika kufahamu mambo unayohitaji kujua.

Category: COMPUTER | Added by: Admin (18/Jun/2013) | Author: Yahyou M. Yahya E W
Views: 3299 | Tags: cd, tofauti, dvd, Computer | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: