Home » Articles » EDUCATION

Kwanini sayari ya Pluto sio sayari tena?

Kwanini sayari ya Pluto sio sayari tena?



Sayari ya pluto ilikuwa ni sayari ya tisa katika mfumo wa jua (Solar System), lakini sasa si hivyo. Tuna sayari nane tu.

Kwanini?

Nilipokuwa shule tulijifunza kuwa sayari ziko tisa, Mercury, Venus, the Earth, Mars, Jupiter, Saturn, Uranus, Neptune and Pluto. Lakini sasa si hivyo tuna sayari chache.

Neno Sayari (Planet) linatokana na neno la kigiriki "Planette” likiwa na maana "nyota ya ajabu” maelfu ya miaka iliyopita wagiriki walipoangalia angani, waliona vinukta nukta vyenye kung’aa angani vingine vikiwa vinatembea (Nyota). Si wagiriki tu ndio walioona hili hata wengine waliona kitu kama hiki. Kila kilichotembea kiliitwa sayari, hivyo wazee wa kigiriki, mwezi, hata jua pia liliitwa sayari. Lakini baadaye ikawa sio hivyo kwani Astronomers waliona kuwa Jua ni Nyota na Mwezi ni Mwezi na si kama ilivyokuwa zamani.

Astronomers waligundua maumbo sita makubwa yaliyofanana na nyota ambazo zilikuwa zikizunguka jua, ambazo ni Mercury,Venus, Earth, Mars, Jupiter na Saturn na ndipo neno sayari likawekwa katika rekodi na ikawa ni kitu cha ajabu hapo zamani.

 

Baada ya masiku mengi kupita sayari zingine zikaanza kugundulika, mnamo mwaka 1781 sayari ya Uranus iligundulika na mwanasayansi aliye uingereza aitwaye Sir Frederick William Herschel  ikifuatiwa na sayari ya Neptune mnamo mwaka 1846, sayari hizi ni kubwa pia na ziko mbali sana ambazo zilifanya Astronomers kupata tabu kuziona.

 

Lakini je unafahamu kuwa mwaka 1881, iligundulika sayari nyingine? Je aliyegundua alifikiri nini?

aligundua vitu vya duara maili 600 kati ya sayari mbili Mars na Jupiter, sayari hiyo ilikuwa ni ndogo sana iliyopewa jina la Ceres hali ambayo ilikuwa ni vigumu sana kuziona kwa jinsi zilivyokuwa ndogo sana, lakini tatizo likajitokeza baada ya muda mfupi pale ilipogundulika sayari nyingine karibu na Ceres iliyojulikana kama Pallas ikifuatiwa tena na njingine iliyojulikana kama Juno na hatimaye kugundulika maelfu ya maumbo kama hayo sehemu hiyohiyo. Badala ya kuwa na maelfu ya sayari katika mfumo huu wa sayari, Astronomers (Astronomers) waliona italeta maana sana ikiwa zitawekwa katika kundi moja na kuziita asteroids. Na hivyo tukafundishwa mashuleni kuwa Asteroids hupatikana baina ya Mars na Jupiter.

 

Kitu kama hikihiki cha asteroid kilitokea tena kwa Pluto, Astronomers katika uchunguzi wao walugundua sayari nyingine karibu na Neptune mnamo mwaka 1930. Hapa ndipo sayari ya Pluto ilipoongezwa katika listi ya sayari zile nane.

Mwanzoni kabisa mwa miaka ya 90 (1990’s) visayari vingine vilianza kuonekana huko karibu na pluto vingine vikiwa na ukubwa sawasawa na Pluto ambavyo viliitwa Quaoar na  Sedna, lakini mnamo mwaka 2005 waligundua kisayari  kingine maeneo hayohayo ambacho ni kikubwa kuliko Pluto kilichoitwa Eris. Hivyo swali likaja sasa Je zote hizo ni sayari? Na kama Pluto ni sayari basi hata yale maumbo mengine makubwa kuliko Pluto yangetakiwa kuwa sayari. Na pia inasemekana kuwa kuna baadhi ya miezi inayozunguka sayari huwa ni mikubwa kuliko Pluto, hivyo hali hii hufanya sifa ya Pluto kuwa sayari iondoke. Hilo ndilo lilikuwa swali kwa Astronomers wote ulimwenguni.

 

Mnamo mwaka 2006 walikutana wote ili kuweza kukubaliana na kupiga kura  kuhusu suala hili na kupata maana halisi ya neno Sayari, ndipo jibu sasa likaja kuwa Pluto haikuwa na sifa ya kuitwa sayari na zote zilizotokea karibu yake na yenyewe ikiwemo zikawekwa katika kundi moja na kuitwa sayari vibete (Dwarf Planets)




Category: EDUCATION | Added by: Admin (13/Apr/2013)
Views: 4644 | Tags: astronomers, elimu, ulimwengu, nyota, Pluto, orbit, sayari | Rating: 1.7/6
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: