Home » Articles » EDUCATION

MAANA YA KUONYESHA V KWA KUTUMIA VIDOLE (V – Sign)

MAANA YA KUONYESHA V KWA KUTUMIA VIDOLE (V – Sign)


 


Alama ya V (V – Sign) ni ishara ya mkono kuonyesha vidole viwili cha kati na cha pili baada ya gumba hali ya kuwa vingine vimekunjwa. Hii ina maana mbalimbali kutegemea na utamaduni wa sehemu fulani na jinsi inavyoonyeshwa. Mara nyingi sana huashiria herufi "V” ikiwa ni kifupi cha neno "Victory” yaani Ushindi.

 

Lakini pia alama hii huleta maana tofauti kutokana na aina Fulani ya uonyeshaji kama ifuatavyo:


  1. Ikiwa upande wa kiganja unamuelekea muonyeshaji wa alama hiyo na upande wa mgongo wa kiganja humuelekea muonyeshwaji  basi hii ni alama ya kutukana. Matumizi haya yamekemewa sana nchini Australia, Ireland, New Zealand, South Africa na Uingereza.

 

Wengi tunapenda kupiga picha kwa kutafuta mapozi haya na yale bila ya kujua maana yake na sanasana ili tuvutie picha zetu wengi huonyesha vidole hivi, ila kumbuka kuwa unapogeuza kiganja chako basi unamtukana huyo anayekupiga picha na wanaokutizama vilevile.  hivyo fahamu hili na usifanye kitu pasi na kujua maana yake.

                       

                                           

 

  1. Ikiwa upande wa kiganja humuelekea muonyeshwaji na mgongo wa kiganja humuelekea muonyeshwaji basi hiyo huonyesha maana tofauti kama ifuatavyo:

 

a)  Aidha huonyesha namba mbili (2) – hii ni aina ya mawasiliano kwa vitendo kumuonyesha mtu. Mfano unaweza kumuuliza mtu miaka ya mtoto wake naye akakujibu kwa vidole hivi, akimaanisha ana miaka miwili.

b)   Maana ya pili ni kama tuliyoizungumzia hapo mwanzo kuwa  inaashiria herufi "V” ikiwa na maana ya "Victory” yaani ushindi.

c)    Utaona pia baadhi ya viongozi wa kimataifa wakionyesha alama hii kwa mikono yote miwili wakiwa na furaha Fulani.

  1. Maana nyingine pia huonyesha kuwa "NIMEKUONA au NAKUANGALIA” ila ishara hii inajulikana pale mtu anapoonyesha vidole hivi kwenye macho yake kisha akavigeuza kumuonyeshea huyo anayemtizama.

Ahsante kwa kuwa pamoja nami na nakutakia siku njema.


Category: EDUCATION | Added by: Admin (08/Jun/2013) | Author: Yahyou M. Yahya E W
Views: 2564 | Tags: victory, ushindi, tukana, v-sign, onyesha, alama | Rating: 1.0/1
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: