Home » Articles » EDUCATION

VIPI KAMA KUNGEKUWA NA CREAM INAYOITWA PHOTOSHOP?

VIPI KAMA KUNGEKUWA NA CREAM INAYOITWA PHOTOSHOP?


Katika ukuaji wa teknolojia, sasa hakuna mgonjwa wa ngozi hata mmoja katika picha zake labda kwa yule asiyejua kutumia kompyuta au hata kufahamu kinachoendelea. Ukweli ni kwamba ni asilimia ndogo sana ya watu hawana chunusi katika nyuso zao. na hata yule ambaye hana basi lazima hatofanana ngozi yake na mtoto mchanga hata kuitwa baby face.

Nani anataka apige picha atishe? Hakuna hata mmoja, kila mtu anataka kupiga picha atokee hali ya kuwa amependeza tena sana. Zamani ilikuwa kazi ngumu sana kupiga picha za urembo ili kumtumia mtu katika matangazo mbalimbali. Lakini sasa ni rahisi sana.


Haijalishi uso wako umeharibika kiasi gani hata ufanane na limao lakini photoshop ndiyo suluhisho la matatizo yote.  Leo ukimuona mtu kapiga picha nzuri sana anapendeza na uso wa kung’aa sana. Lakini kumbe kuna marekebisho makubwa sana yamefanyika katika kuleta matokeo hayo mazuri tena yenye mvuto.


Kwa kutumia photoshop unaweza kupiga picha hali yoyote ile uliyonayo na kisha ukatumia hii program katika kuondoa kila usichokipenda katika uso wako, yakiwemo madoa na chunusi. Hii imesaidia sana kupunguza gharama na muda wa mtu kukaa na kujipamba ili apige picha za matangazo mbalimbali.

Ina faida kubwa kama nilivyoieleza hapo lakini pia kuna wakati inatakiwa itumike katika hali ya kuangalia matokeo ya baadaye. Nadhani hapo unaweza kujiuliza nimemaanisha nini. Iliwahi kutokea mmoja kafanya marekebisho makubwa sana ya picha zake na kuziweka katika mtandao wa kijamii Facebook. Kisha baada ya muda fulani akajenga uhusiano na kijana waliyejuana naye humo humo ndani ya Facebook.

Kweli kijana alimpenda sana kwani alikuwa anavutia na mwenye ngozi nzuri yenye mvuto wa kila hali. Ila sasa mabadiliko yalikuja pale walipoahidiana kuonana. Nadhani hapo utajua jibu lilikuwa vipi baada ya kuonana. Ukweli ni kwamba kila zuri likitumika bila uangalifu na manufaa ya baadaye linaweza kutuletea madhara.

Program hii ni nzuri sana na ndiyo yenye nguvu ya kuhariri picha (photo editing), imewaletea kipato watu wengi sana kuanzia watumiaji hadi wafundishaji wa program hii. Kweli ukiangalia jinsi picha zinavyorekebishwa na kufanya ngozi iwe nzuri unaweza kusema "Vipi kama kungekuwa na Cream inayoitwa Photoshop?” hapo wote tungekuwa na ngozi ya kitoto na tungevutia tena sana.


Lakini haiwezekani, kila mtu ana afya yake, ana hali yake ya maisha na vyakula anavyokula hivyo ubora wa ngozi yako unategemea na afya yako jinsi unavyoitunza. Kama kweli unapenda kuitunza ngozi yako iwe kama ile iliyofanywa na Photoshop basi inawezekana tena cha msingi ni wewe tu kujua hatua gani za kudumisha Afya ya ngozi yako.

Sina mengi kwa hayo, nakutakia kila la kheri katika kujifunza elimu mbalimbali na manufaa katika tovuti yetu hii. Ikiwa una swali jisikie huru. Tupo pamoja.

 

Category: EDUCATION | Added by: Admin (01/Jul/2013) | Author: Yahyou M. Yahya E W
Views: 1497 | Tags: Photoshop, cream | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: