Home » Articles » HEALTH

FAIDA NA MADHARA YA KULA PILIPILI MANGA

FAIDA NA MADHARA YA KULA PILIPILI MANGA

 

Pilipili manga ni mbegu ndogondogo zenye umbo la mviringo zenye rangi nyeusi.mbegu hizi hutoa ladha ya muwasho mfano kama pilipili na kutumika sana majumbani hasa upande wa jikoni, wapo wanaotumia kiungo hiki kikiwa kizima au kimesagwa inategemea na mtumiaji anavyopendelea.

 

Wanawake wengi wa pwani hutumika pilipili manga  katika vyakula ili kunogesha na kukipa ladha iliyo nzuri chakula, kitoweo hata kinywaji. Pia wapo wanaotumia pilipili manga kuramba endapo watahisi kifua kinawabana. Licha ya kuwa pilipili manga si dawa ya kifua ila kwa mazoea tumeipa nafasi pilipili manga kuwa ina uwezo wa kutibu kifua kama ifanyavyo tangawizi.

 

Faida ya matumizi ya pilipili manga kwa wanawake.

 

Pilipili manga ina faida kubwa kwa mwanamke ambaye ameshajifungua, hivyo ni vema uji anaokunywa uwekwe unga wa pilipili manga kwani humsaidia kutoa uchafu utakaokuwa upo kwenye kizazi ambao umebakia.

 

Humuondolea maumivu ya mwili pamoja na tumbo, humsaidia kutoshika mimba katika kipindi hicho ambacho analea mtoto wake mchanga. Wapo baadhi ya watu wakila chakula au mchuzi rosti wa biriani ambayo inakuwa haijachanganywa na kiungo hiki hupata ugonjwa wa kuharisha au kupata maumivu makali ya tumbo.

 

Lakini endapo utaweka pilipili manga kiasi kidogo basi mtu huyo hatoweza kuharisha wala kuumwa na tumbo hivyo kwa upande mwingine kiungo hiki huisaidia kutibu tumbo kwa mlaji. Katika matumizi ya watu wengi inashauriwa itumike pilipili manga ambayo ni nzima ili mtu ambaye inamdhuru akiwa anakula chakula ni lazima ataona vitumba vya pilipili manga na kuviondoa.

 

Madhara ya matumizi ya pilipili manga;

 

Kwa mwanamke anayehitaji kupata mtoto haruhusiwi kutunmia kiungo hicho kwa wingi kwani kinaweza kumsababishia kushindwa kushika ujauzito na hivyo kuhangaika kwa muda mrefu licha ya kutumia dawa za kila aina. Mwanamke yeyote ambaye anahitaji kupata mtoto anatakiwa ajichunge sana na vyakula anavyokula kwani viko vyakula vingine vina uwezo wa kumsababishia kushindwa kushika ujauzito kwa urahisi.

 

Usitumie pilipili manga kutibu kifua. Kiungo hiki kinapoliwa na mgonjwa wa kifua humsababishia kukohoa mara mbili zaidi ya hapo awali. Kutokana na muwasho, kiungo hiki kuingia moja kwa moja kwenye mapafu na kusababisha mkwanguo ambao unaweza kuleta madhara ya mgonjwa kukohoa damu.

 

Wapo wanaotumia maji ya limao na pilipili manga pindi wanapokohoa. Ni vema waache mara moja. hii ni hatari sana. Pia kiungo cha pilipili manga husababisha ugonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa ambao hupenda kunywa uji uliotiwa pilipili manga kwa wingi wakitumia kama ndio kifungua kinywa.

 

Elewa kuwa utumbo ni laini sana hivyo ni vizuri kujijali hasa katika matumizi ya vyakula vyenye pilipili chache na nyingi kabla ya kula chakula chochote. Hukatazwi kunywa uji wenye pilipili manga ila unatakiwa kuweka kiasi kidogo sana cha kiungo hicho ili kukuepusha na madhara ya vidonda vya tumbo.

 

Angalizo:

 

Wanawake waliokuwa ndani ya ndoa punguzeni matumizi ya pilipili manga na hatimaye ongezeni matumizi ya mdalasini. Mdalasini unaweza kutumiwa  kwa  jinsi zote ukiwa mapande mapande au umesagwa na kuwa unga. Unga wa mdalasini huchanganywa na asali kisha watumiaji wale kijiko kimoja cha chakula asubuhi, mchana na jioni. Hii itamsaidia sana katika suala la kupata mtoto, watu waliogundua matumizi ya pilipili manga katika kipindi cha kujifungua hawakuwa wajinga kwani kiungo hiki kilikuwa kinatumika enzi na enzi za babu na bibi zetu.

 

Kwa maoni, maswali na ushauri jisikie huru kutuandikia katika kisanduku hapo chini.

 

Category: HEALTH | Added by: Admin (27/May/2013)
Views: 26875 | Tags: hasara, pilipili, faida, manga, ujauzito, mimba, afya | Rating: 2.1/26
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: