Home » Articles » HEALTH

HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIYEPATWA NA PRESHA YA KUSHUKA


HUDUMA YA KWANZA KWA MTU ALIYEPATWA NA PRESHA YA KUSHUKA



Maisha yamejaa mambo ya kushangaza na vitu vingi vigeni. Hata hivyo, kwa kuwa na elimu nzuri na iliyosawa kabisa mtu anaweza akarekebisha matatizo yanayoweza kutokea ghafla.

Presha ya kushuka:

Presha ya kushuka (Low Blood Pressure (BP)), au kwa lugha ya kisayansi huitwa Hypotension. Hali hii inatokea pale msukumo wa damu unapokuwa mdogo na dhaifu, hali ambayo husababisha kila kiungo katika mwili kama vile ini, mapafu, moyo nk. Kushindwa kupokea kiasi kinachojitosheleza cha damu na Oxygen.


Sababu za Presha ya Kushuka:

·         Mshtuko

·         Ukataji tama

·         Mawazo mengi yaliyopitiliza

·         Mlo usio kamili – vitamin, Protini na ukosefu wa madini

·         Ukosefu wa maji mwilini.


Dalili:

·         Udhaifu usioutegemea (ghafla)

·         Udhaifu au kuona ukungu.

·         Mdomo kukauka

·         Kizunguzungu

·         Kuanguka ghafla na kupoteza fahamu.


Huduma ya kwanza:

Kama mtu ataanza kusikia kizunguzungu, muweke akae katika kiti au mlaze chini.

·         Mnyanyue kichwa chake wakati ukiwa umemlaza chini, kwa kumuwekea mito chini ya kichwa chake.

·         Haraka mnyweshe maji uliyochanganya na chumvi au mpatie mgonjwa huyo electrolyte solution.

·     Kuwa makini unapomuinua kutoka chini au sehemu aliyokuwa amekaa. Muinuko wa ghafla unaweza kuzidi kupunguza msukumo wa damu.

·      Hali ikidumu kwa muda mfunge mgonjwa katika mguu wake umbali wa nchi kama tano hivi  chini ya goti kwa kutumia lastiki au mpira unaovutika ili kuzuia damu isiende chini ya miguu, ili kufanya damu ibakie hasa sehemu ya juu ya mwili.

·         Kunywa juisi ya kiazisukari kibichi au maziwa ya mtindi ni dawa nzuri ya presha ya kushuka.

Onyo:

·         Punguza kunywa Vinywaji vya alcohol au kafeini

·         Jitahidi kuwa unakula matunda freshi na mbogamboga katika mlo wako

·         Jitahidi kunywa maji mengi ili kuepuka ukosefu wa maji

·         Usipende kunyanyua mizigo mizito sana.

·         Chukua mazoezi kwa ratiba maalum.



Kumbuka dharura huwa hazipigi hodi zinapokuja katika maisha yako. Hivyo basi, siku zote kuwa ni mwenye kujiandaa. Wakati mwingine matendo madogo madogo na kuwa na akili iliyotulia inaweza ikaokoa uhai, mpaka pale dharura za kitabibu zitakapofika.


Usikose makala ijayo kujua ni jinsi gani unaweza kumsaidia mtu aliyepatwa na presha ya kupanda.

Ahsante kwa kuwa pamoja nami.


unaweza kutoa maoni yako hapa au kuchangia lolote unalojua zaidi kuhusu mada hii.



Category: HEALTH | Added by: Admin (09/Mar/2013)
Views: 14056 | Comments: 1 | Tags: msukumo wa damu, presha ya kushuka, moyo | Rating: 2.0/17
Total comments: 1
1 Salama seif  
0 Spam
I love the web

Name *:
Email *:
Code *: