Home » Articles » HEALTH

UKOSEFU WA USINGIZI

UKOSEFU WA USINGIZI

Hali zote mbili huweza kukukosesha usingizi iwe shida au raha iliyozidi

 

Ukosefu wa usingizi ni tatizo kubwa sana linalowakumba watu wengi hivi sasa, unaweza kujiandalia mazingira ya kulala ili upumzishe akili yako na kujiandaa na siku mpya lakini hali inakuwa tofauti pale unapojiweka kitandani ili upate usingizi.

 

Unaweza kukaa hata zaidi ya nusu saa na usipate usingizi kabisa hali inayomfanya mtu apate tabu sana na kuumiza afya yake. Tatizo hili limewatesa watu wengi sana na kuwaharibia ratiba zao nyingi kutokana na kuchelewa kupata usingizi na hatimaye kulala usiku wa manane hali inayopelekea kwa bahati mbaya mtu kupitiliza muda maalum wa kuamka.

 

Nini hasa sababu ya tatizo hili?

 

Kuna sababu mbalimbali zinazosababisha ukosefu wa usingizi zikiwemo sababu nzuri na mbaya. Kama zifuatazo.

 

  1. Kujawa na msongo wa mawazo.

Unapokuwa na mawazo mengi sana husababisha kushindwa kupumzisha akili yako kwani muda wote unakuwa uko macho na kufikiria juu ya mambo fulani.

 

  1. Kuwa na hofu na wasiwasi.

Ukiwa  ni mtu mwenye hofu na wasiwasi siku zote hutokuwa na usingizi mzuri kabisa na matokeo yake kujidhuru kiafya na kupata matatizo ya moyo, jiepushe sana na wasiwasi kwani itakugharimu afya yako. Na kumbuka kuwa huenda ukawa una wasiwasi bure tu bila ya sababu yoyote. Hii hutokana na kutawaliwa na akili yako kwa kushindwa kuidhibiti kufikiria hili na lile.

 

  1. Hali ya hewa isiyofaa

kwa asilimia kubwa sana ndani ya mwaka huwa ni kipindi cha joto kali sana na hasa katika mikoa ya pwani kama vile Tanga, Dar es salaam, Pwani n.k hali hii husababisha pumzi kuwa nzito wakati unalala na kutokwa na jasho jingi hali ambayo inasababisha mtu kuona kero katika usingizi. Ndio maana kuna baadhi ya sehemu watu huamua kulala nje ili wapate hewa iliyo nzuri.

 

  1. furaha na matarajio yaliozidi

unaweza kuwa na furaha sana, labda umefaulu mtihani, umepata kazi, umepata pesa nyingi hivyo kuwa macho muda wote, na hata ukijitahidi kulala huwezi kwani akili haikubali kupumzika kufikiria juu ya suala hilo. Au unaweza kuahidiwa kitu fulani ambacho maishani mwako kukipata ni kama ndoto, hivyo hali hii inaweza kukuweka muda wote macho na hali ya uchovu na usingizi kutoka kabisa, na unaweza kuona masaa hayaendi kabisa ili asubuhi ifike.

 

  1. Maradhi na matatizo ya kiafya

Vilevile maradhi na matatizo ya kiafya huweza kusababisha mtu kukosa usingizi kabisa kwani unaweza kuwa na homa kali, au maumivu sehemu fulani. Basi hali kama hii inaweza kukufanya ukose usingizi kabisa na ndio maana wagonjwa wengi hupewa dawa za usingizi ili waweze kupumzika.

 

Fahamu ya kwamba usingizi haukosekani kwa matatizo tu bali hata kwa raha vilevile kama tulivyoelezea hapo juu.


Usingizi ni jambo zuri sana na hujenga afya yako na kuboresha nguvu ya fikra zako hivyo jitahidi sana uepukane na kila jambo ambalo linaweza kukukosesha usingizi kwani unaweza kukosa kufanya mambo mengi ya muhimu kwa kukaa macho usiku kucha na kujikuta ukiumia kichwa muda wote.

 

Ikiwa una swali juu ya mada hii usisite kutuuliza kwani tunajitahidi katika kuelimisha jamii yetu. Na pia usisite kutuandikia maoni yako ikiwa unayo.

 

Category: HEALTH | Added by: Admin (02/Jun/2013)
Views: 1148 | Tags: mawazo, raha, shida, amka, uchovu, afya, usingizi, usiku, Lala, ukosefu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: