Home » Articles » HEALTH

UVUTAJI WA SIGARA NA TUMBAKU

UVUTAJI WA SIGARA NA TUMBAKU



Uvutaji wa sigara kama mazoea

Kama unavuta sigara kwa lengo la kukupoza pale unapohisi una msongo wa mawazo; kama hujisikii vizuri asubuhi mpaka upige pafu (uvute japo kidogo); kama unajisikia mfadhaiko, uchovu na kuumwa na kichwa ikiwa hujavuta sigara na pia ukajihisi kuwa huwezi kuzingatia jambo mpaka uvute sigara, basi ujue ya kwamba umetawaliwa sana na uvutaji wa sigara. Je kitu gani kinachofanya watu mpaka watawaliwe na uvutaji?

Hii ni kwasababu wametawaliwa na athari ya Nicotine (Sumu iliyo katika Tumbaku)  katika ubongo. Nicotine hutoa raha fulani ya muda mfupi kwa mvutaji pale anapopiga pafu. Na muda huo huo raha hiyo huondoka.  Hivyo basi ili mvutaji aendelee kupata raha hiyo, humfanya apige pafu nyingine zaidi ili kuendelea kupata raha zaidi na zaidi. Hivi ndivyo Nicotine humfanya mtu apate mazoea na kutawaliwa na uvutaji.

Hivyo basi, mvutaji akishatawaliwa na tabia hii, uvutaji huu utamfanya mtu aepukane na tabia fulani kama vile hasira, hamu, ugumu wa kuzingatia, njaa, ukosefu wa subira na mengineyo kwasababu sigara imekuwa ni kama sehemu fulani katika maisha ya kila siku.

Nicotine huondoka haraka sana mwilini katika masaa machache, hivyo mvutaji hujikuta akiendelea kuvuta masaa kadhaa kwa siku ili aendelee kupata msaada huo wa Nicotine katika mwili wake. Kwa wastani, wavutaji waliotawaliwa na uvutaji wa sigara huvuta kuanzia sigara 10 hadi 50 kila siku. Nicotine huweza pia kuingia mwilini kwa njia nynginezo kama vile kula tumbaku yenyewe kama wengi wafanyavyo sasa.

Jinsi Nicotine inavyofika katika ubongo

Uvutaji wa sigara hutengeneza njia ya haraka sana katika ubongo, unapovuta sigara ile pumzi huingia na Nicotine katika mapafu na kusambaa katika damu haraka sana kabla hata hujaitoa nje. Vile vishipa vidogo vilivyozunguka vifuko vidogo vya hewa  huwezesha damu katika mwili kupita katika mapafu kwa takriban lita tano kwa dakika.

Kutoka katika mapafu, damu yote huenda upande wa kushoto wa moyo. Kutokea huko pindi inapotolewa nje, kiasi fulani cha nicotine huenda katika ubongo. Hivyo ubongo hupata unyevu wa kimiminika kipya cha nicotine haraka sana baada ya kuvuta mpigo mmoja tu. Nicotine hufika katika ubongo wa mvutaji haraka sana kuliko hata inapoingia katika mishipa ya damu na ndio maana ndani ya sekunde 6 mpaka 8 mvutaji anakuwa ameshahisi athari ya uvutaji wake.

Kwa kuwa nicotine hufika katika ubongo kwa kiwango kidogo kidogo. Hivyo mvutaji anakuwa na hamu ya kuendelea kuvuta. Kwa hisia zaidi, mvutaji huendelea kuvuta zaidi na zaidi. Ikiwa sumu ya nicotine itazidi katika ubongo kwa ile hali ya kuvuta sana. Mvutaji hujisikia kizunguzungu na kichefuchefu na huacha kuvuta au kupunguza.

Jinsi  nicotine inavyofanya kazi  kwenye ubongo na katika akili.

Nicotine hufanya kazi ya kuchochea neurotransmitters na neurohormones katika ubongo. Kwa dozi ndogo tu, nicotine huchochea kutolewa kwa beta – endorphin, hii ni ile dawa ya kutuliza au kuleta pozo katika mwili. Na hivyo mvutaji hujihisi ametulia na kustarehe kabisa.

Kinyume chake kwa wale wavutaji waliobobea, hii nicotine huchochea nonadrenaline, adrenaline na dopamine. Mvutaji hujihisi raha na mtulivu au kujiona yuko katika hali nzuri ya kifahari.

Inabidi ieleweke kuwa hizi neurotransmitters au hormones huchochea kituo cha furaha katika ubongo na kumfanya mvutaji atawaliwe na uvutaji.

Nicotine pia imepasishwa kuchochea uwezo wa kiakili kutokana na kuongezeka kwa neurotransmitters ambazo zinahusika na kazi ya kumbukumbu – Acetylcholine na Vasopressin.

Hatahivyo, hizi athari za vichocheo ambavyo unaweza kuviona, havidumu kabisa, kutoka dakika 15 mpaka 30. Hivyo faida hizi ni za muda mfupi sana wakati madhara yake ni mengi na makubwa kama tulivyoeleza katika makala hii Bofya hapa kuisoma na ujue madhara haya ya uvutaji.

 

Category: HEALTH | Added by: Admin (12/Jul/2013) | Author: Yahyou M. Yahya E W
Views: 1494 | Tags: tumbaku, sigara, nicotine, madhara, uvutaji | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: