Home » Articles » WEBSITE DESIGNING

SOMO LA KWANZA: HTML INTRODUCTION

SOMO LA KWANZA:  HTML INTRODUCTION

 

Nini maana ya HTML?

HTML ni lugha inayotumika katika kutengenezea tovuti (web pages).

  • HTML stands for Hyper Text Markup Language
  • HTML is a markup language
  • A markup language is a set of markup tags
  • The tags describe document content
  • HTML documents contain HTML tags and plain text
  • HTML documents are also called web pages

Katika HTML kuna kitu kinajulikana kwa jina la HTML Tags, je nini maana yake? Na hutumiwaje?

Unapotumia html lazima utumie hiki kitu kwani bila ya Html tag huwezi kufanya lolote kwani ndio ufunguo wa lugha hii ya kutengenezea website. Html Tag inakuwa katika mfano kama huu <name>  ikiwa na maana kuwa ufungo wa neno unakuwa katikati ya mabano hayo yenye pembe (angle brackets).

 

HTML Tags huwa mara nyingi huja kwa jozi, yaani kama kuna <name> basi lazima kuwe kuna </name> ikiwa na maana kwamba, ile ya kwanza ni ya kufungua na ya pili ni ya kufunga.

 

 Ila kumbuka kuwa tag ya mwisho ambayo ndiyo ya kufunga huwa inafanana na ile ya kufungua isipokuwa tu hii ya kufunga lazima ianze na alama ya mkwaju "/” kabla ya kumalizia neno husika. Mfano <name>……………</name> na huwezi kukuta kitu kama hiki <name>……..<name> au <name>………….</example>.

 

HTML ELEMENT

 

Hii ni kila kilichopo baina ya tag mbili pamoja na tag zenyewe. Mfano <tag> this is my first page</tag>

Hivyo basi, ukikutana na sentensi kama hiyo <tag> this is my first page</tag> basi ujue kuwa hiyo ni HTML Element.

 

Kumbuka kuwa kazi ya tag ni kuamrisha yale maneno yaliyo baina ya tag hizo mbili, kuwa kwa jinsi tag hizo zilivyohitaji. Nitakupa mfano lakini sio katika HTML ila nimetumia mbinu hii ili kukuelewesha. Tuchukulie mfano unataka maandishi yako yatembee, maandishi yenyewe labda ni haya "KARIBU SANA” na katika ujuzi wako ukaona kuwa tag inayofaa kuamrisha maandishi yatembee inaitwa <tembea>, hivyo basi katika kutengeneza kwako utaandika kama ifuatavyo:

 

<tembea>KARIBU SANA</tembea>

 

Kwa mfano huo hapo juu neno "KARIBU SANA” litaanza kutembea pale utakapoijaribu  tovuti yako. Lakini hakuna tag inayosema hivyo huu ni mfano halisi wa kukuelewesha tu jinsi HTML tag zinavyofanya kazi.

Na kama ukisahau kufunga tag basi hakuna matokeo yoyote utakayoona mfano umeweka <b>My first page. Hapo hujafanya kitu kwani hakuna Close Tag. Ni usahihi wake kuwa hivi <b> My first page </b> hivyo kuwa makini juu ya hili.

 

Sasa je tunaanza vipi kuandaa ili tuanze kuandika website yetu?

Kuna program zinazotumika kuandikia tag zetu ili tuweze kutengeneza website kama vile,

  • Adobe Dreamweaver
  • Microsoft Expression Web
  • CoffeeCup HTML Editor

Lakini kwa kujifunza HTML nasisitiza sana kutumia Notepad na ni njia rahisi na bora sana katika kujifunzia kuliko kwenda mbali huko. Nadhani kila mtu anajua kuwa katika Windows kuna program ndogo inayoitwa notepad, program hii kazi yake sana utaona ni kuandikia maneno lakini ina umuhimu mkubwa sana kwani hutumika kutengeneza baadhi ya application ndogo ndogo za kompyuta. Hivyo kwa hii hii tutaitumia katika kutengeneza web page.

 

Kwa asiyejua kuifungua hii fuata maelekezo haya:

To start Notepad go to:

Start
    All Programs
        Accessories
            Notepad

Baada ya hapa notepad itafunguka. Muonekano wake ni kama huu hapa chini:

 


 

Sasa hapo ndipo tunapoandika HTML Tags ili kufanikisha utengenezaji wa web page. Ni kama ndoto kwani hakuna lolote litakalowekwa humo ndani isipokuwa ni maandishi tu, lakini itatokea kurasa nzuri kabisa ya tovuti.

 

Kuwa pamoja nami somo lijalo tuone jinsi gani ya kuanza kuandika webpage yetu hapo.



Category: WEBSITE DESIGNING | Added by: Admin (10/Apr/2013)
Views: 1136 | Tags: website, somo la kwanza, notepad, html, tovuti | Rating: 1.7/3
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: