Home » 2017 » October » 13 » Alibaba na wezi 40 Part 5
18:26
Alibaba na wezi 40 Part 5

SEHEMU YA TANO

Sura ya tatu

MAITI PANGONI

Kutoka sehemu ya nne:

Baada ya Kassim kwenda pangoni kwaajili ya kujipatia dhahabu na mali nyingi, kwa bahati mbaya alisahau neno la siri la kufungulia lango la pango wakati yuko ndani, hivyo alishindwa kutoka nje ya pango na hatimaye kukutwa na wezi wale wenye mali zao na kumuua. Baada ya kumuua wezi wale wakagundua kuwa sio Kassim peke yake anayejua mali zao na kuziiba, bali kuna mtu mwingine. Hivyo wakaamua kuuning’iniza mwili wa Kassim pangoni ili yule mwingine atakayekuja iwe ni somo kwake na onyo.

 

ENDELEA SEHEMU YA TANO

Siku nzima mke wa Kassim alikaa dirishani akimsubiria mumewe atoke huko pangoni. “Uko wapi Kassim?” alijisemea mwenyewe,”Uko wapi?, kwanini usingebaki na mimi huku? Kwanini ulienda pangoni kutafuta dhahabu?” yote haya alijisemea ingawa hajui kilichotokea huko pangoni.

Mpaka jua lilipozama, mke wa Kassim akaona sasa si muda wa kukaa na kusubiri, lazima kutakuwa na tatizo tu. Akakimbia haraka kwa Alibaba na kugonga mlango.

Alibaba alipofungua tu, aliingia ndani na kuanza kulia. “Alibaba nisaidie, kaka yako tangu alipoondoka asubuhi leo hajarudi mpaka sasa hivi kutoka pangoni! Aliondoka kabla jua halijachomoza vizuri na punda kumi, aliniambia anaenda huko kuchukua dhahabu, nilikaa dirishani kumsubiria siku nzima, nadhani kuna jambo baya limemtokea huko, tafadhali nisaidie, Alibaba! Tutafanya nini?”

“Usihofu,” alijibu Alibaba, “Nitakwenda na punda huko msituni kumtafuta. Nenda nyumbani na unisubirie, nitarudi muda sio mrefu na nakuahidi kwamba nitakuja na kaka yangu.”

Hivyo basi Alibaba alichukua punda wake watatu na kuelekea msituni. Wakati anaendelea kwenda msituni, Alibaba alikuwa akimtafuta kwenye miti miti huku akiita jina lake, lakini hakuona wala kumsikia mtu yeyote. “simpati Kassim, wala punda wake kumi pia siwaoni” Alibaba alijisemea. “Kassim aliweza kujua lile pango lilipo? Je aliweza kupata dhahabu? Mh! Huenda mkewe akawa yuko sahihi labda mumewe kuna jambo baya limemtokea.”

Alibaba alipokaribia pangoni, aliona michirizi ya damu ardhini. “hii ni ishara mbaya!” alifikiria. Kisha akasema, “nitaenda pangoni nikaangalie kama Kassim yupo mle ndani”. Aliwaacha punda wake watatu chini ya mti kisha akasogea mpaka karibu na lango la pangoni kisha akasema lile neno la siri, “Fungukaaaa sesmiiiii!!!

Lango lilipokuwa likifunguka taratibu, Alibaba aliona kitu chenye kushtua sana. Aliona mwili wa mtu ukining’inia juu ya pango, alipokaribia kuutazama kwa karibu zaidi akaona kuwa ni kaka yake, Kassim. Alibaba alianguka chini kwa magoti na kuanza kulia. “Masikini Kassim!!” alisema! “alikuwa ni mwenye tamaa, lakini ni kaka yangu. Ona sasa kundi la wezi limemuua kwasababu ya tamaa!!”

Alienda ndani ya pango zaidi na kupata dhahabu zilizofungwa na nguo kubwa nyeupe. Alizitoa dhahabu zile na kuchukua ile nguo kubwa kisha akaufunga mwili wa kaka yake latika nguo ile, kisha akaubeba mwili wa kaka yake mpaka kwenye punda mmoja kati ya wale watatu aliokuja nao. Kisha  akaufunika mwili ule na baadhi ya kuni ili usionekane na watu njiani. Alibaba hakutaka watu wajue kuhusu hazina zile ndani ya pamoja na wezi 40. Kisha akarudi ndani ya pango.

“Nitachukua kiasi kidogo cha dhahabu zaidi,” alisema Alibaba, “kiasi cha kujaza makapu manne niliyokuja nayo na wale punda wangu.”  

Alijaza dhahabu kwa punda wawili kisha akazifunika na kuni kisha akasema neno la siri la kufungia pango, “Fungaaaaa sesmiii!!!” na kisha akaondoka.

Alipofika nyumbani, mkewe Alibaba alikuwa akimsubiria. “Kaka yangu amekufa,” Alisema Alibaba. “Nataka niupeleke mwili wake kwa mkewe sasa hivi.”

“Oooh masikiti Kassim, kimetokea nini huko?” Alisema mke wa Alibaba. “aliweza kwenda pangoni na kuchukua dhahabu?”

“Alikwenda pangoni,” alisema Alibaba. “lakini aliuliwa. Nafikiri wezi waliwahi kurudi na kumkamata. Walimuua kwasababu alitaka kuiba mali zao.”

“Oooh masikini,” alisema mke wa Alibaba. “lakini alitaka dhahabu kidogo tu, na hiyo imemgharimu maisha yake.”

“Usimwambie mtu yeyote kuhusu hili,” alisema Alibaba. “Sasa wacha mimi niupeleke mwili wa Kassim kwa mkewe, lakini, wakati mimi nimeondoka, chukua hizi dhahabu nilizokuja nazo na uzifukie pamoja na zile zingine.”

Mke wa Alibaba akachukua dhahabu na jembe tayari kwa kwenda kuzifukia, na huku alibaba alimchukua yule punda alioubeba mwili wa kaka yake na kwenda kwa mkewe.

Endelea sehemu ya sita.....

 

Category: Stories & Entertainment | Views: 269 | Added by: Admin | Rating: 1.0/1
Total comments: 4
4  
Fantastic

3  
Nzuri sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa smile smile smile smile smile smile

1  
Can't wait more....pls no. 6

0
2  
Dont worry... No.6 is around the corner

Name *:
Email *:
All smileys
Code *: