Home » Articles » COMPUTER

JINSI YA KU-LOCK FOLDER BILA YA PROGRAM


JINSI YA KU-LOCK FOLDER BILA YA PROGRAM

 

 

 

Katika upande mwingine leo tutaangalia njia rahisi ya kuficha au ku-lock folder ili lisiweze kufikiwa na watumiaji wa kompyuta yako.

 

Njia hii ni rahisi sana kwani haihitaji kutafuta program ya kukusaidia kulock folder lako, unachohitaji ni wewe tu kuwa katika computer yako basi.

 

Kwa lugha rahisi sana ambayo naweza kutumia ni kukueleza kwamba, unachotakiwa ni kuwa na ufunguo (key) wa kufunga na kufungulia folder kama vile mtu anavyotumia ufunguo wake kufunga na kufungulia mlango wa nyumbani kwake.

 

Hivyo basi, hebu tuanze kuutengeneza huu ufunguo wetu kwanza.

 

Hatua 1:

Copy hizi code hapa chini katika jedwali letu, halafu fungua Notepad kisha kazipaste hapo.

 

@ECHO OFF
title Folder Locker
if EXIST "Control Panel.{21EC2020-3AEA-1069-A2DD-08002B30309D}" goto UNLOCK
if NOT EXIST Locker goto MDLOCKER
:CONFIRM
echo una uhakika unataka kulifungua hilo folder?(Y/N)
set/p "cho=>"
if %cho%==Y goto LOCK
if %cho%==y goto LOCK
if %cho%==n goto END
if %cho%==N goto END
echo Invalid choice.
goto CONFIRM
:LOCK
ren Locker "Control Panel.{21EC2020-3AEA-1069-A2DD-08002B30309D}"
attrib +h +s "Control Panel.{21EC2020-3AEA-1069-A2DD-08002B30309D}"
echo Folder locked
goto End
:UNLOCK
echo Enter password to Unlock folder
set/p "pass=>"
if NOT %pass%==type your password here goto FAIL
attrib -h -s "Control Panel.{21EC2020-3AEA-1069-A2DD-08002B30309D}"
ren "Control Panel.{21EC2020-3AEA-1069-A2DD-08002B30309D}" Locker
echo Folder Unlocked successfully
goto End
:FAIL
echo Invalid password
goto end
:MDLOCKER
md Locker
echo Locker created successfully
goto End
:End

 

 

 

Hatua ya 2:

weka password unayohitaji kwa kuhariri mstari huu wa code

 

if NOT %pass%==type your password here goto FAIL

 

na kuondoa neno type your password here  kisha weka neno lako la siri. Kwa mfano ikiwa inahitaji password yako iwe 12345 basi huo mstari utakuwa kama hivi:

 

if NOT %pass%==12345  goto FAIL

 

Hatua ya 3:

Save as…. locker.bat hakikisha sehemu ya chini ya kuweka file type iwe all files, na ujue sehemu ambayo hili file la locker.bat litakapofikia baada ya kusave. kisha bofya kifungo cha neno Save kilichopo upande wa kulia. Angalia picha hapa chini:

 

 

 

Hatua ya 4:

Nenda sehemu uliposave file hili la Locker.bat. Baada ya hapo ufunguo wetu huu "locker” utaonekana sehemu uliposave.

 

Sasa basi tayari tumeshatengeneza ufunguo, tunachohitaji sasa ni chumba cha kuhifadhia mafaili yetu ambayo ufunguo wake ndio huo tulioutengeneza.

 

Unachotakiwa sasa ni ku-double click ufunguo wetu. Na baada ya hapo litajitengeneza folder lenye jina kama lile la ufungo wetu ambalo ni "Locker”. Humo sasa utaweka mafaili yako yote ambayo unahitaji yasionekane na watu wengine wanaotumia hiyo computer.

 

Kisha uta-double click tena katika ufunguo wako ili kulifunga folder hilo. Itatokea command kukuuliza kama una uhakika unataka kulifunga folder hilo, kama unataka kweli kulifunga kwa wakati huo basi utaandika herufi moja tu "y” kisha utabofya ENTER katika Keyboard, na ukishamaliza hapo hilo folder litapotea kabisa halitaonekana. Utaulizwa hivyo kila wakati utakapotaka kulifunga folder lako hilo.

 

Kulifungua tena ili lionekane uta-double click katika ufunguo wako kisha itatokea command kukuuliza password ya kufungulia folder hilo. Ukipatia, folder litaonekana, na kama ukikosea basi halitaonekana.

 

Ikiwa utahitaji kubadilisha password, unaweza kufanya hivyo kwa kuhariri (edit) code za ufunguo huo kama tulivyofanya katika hatua ya pili hapo juu.

 

ili uzione code zako tena unachotakiwa ni ku-right click katika ufunguo wako "Locker” kisha Edit, hapo itafunguka notepad ikiwa na hizo code za ufunguo wako. Baada ya kubadilisha utasave code yako. (kumbuka unaposave faili mara ya pili hatutumii Save As… bali utatumia Save kwani tayari faili lako lipo).

 

MUHIMU:

 

Usiache ufunguo wako hapo kwani akitokea mjuzi anaweza kufungua mafaili yako hapo au kukubadilishia password, hivyo ni vema ukaliondoa sehemu hiyo na kuficha sehemu yoyote ile unayopenda.

 

Hata kama utalifuta kabisa basi haitakuwa vibaya kwani unaweza kutengeneza jingine cha msingi tu uweke password kama ile ya mwanzo.

 

Pia usibadilishe Jina la folder lako kwani ukibadilisha ufunguo hautafanya kazi hapo na matokeo yake utatengeneza folder jingine kabisa. Na ikiwa umebadilisha kwa bahati mbaya basi ni vema uhakikishe umerudisha jina la zamani "Locker”

 

Mbinu hii hutumia Show and Hide attribute hivyo hakikisha umeweka Do not show hidden files and folders katika control panel >> Folder options katika menu ya Show.

 

Kwa maswali zaidi na maoni yako jisikie huru kutuandikia. Kwa kutaka pia kufahamu mengi na kuchangia mada mbali mbali jiunge nasi na uwe mwanachama na ukutane na marafiki mbalimbali ulimwenguni, This is Informative.



Category: COMPUTER | Added by: Admin (23/Aug/2013)
Views: 3230 | Comments: 2 | Tags: ufunguo, funguo, Lock, jinsi, folder, attribute, notepad, Code | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: