Home » Articles » COMPUTER

MAANA YA HTTP (Hyper Text Transfer Protocol) na Jinsi inavyofanya kazi:

MAANA YA HTTP (Hyper Text Transfer Protocol) na Jinsi inavyofanya kazi


Katika usomaji mzima wa mambo ya tovuti (website) utakutana na kitu hiki "http”, na mara nyingi utaona kuwa kila website lazima ianze kwa http, mfano: http://www.staryte.ucoz.com/ lakini unaweza kujiuliza hii HTTP ni nini? Na kwanini?

Http ina maana ya Hyper Text Transfer Protocal yaani ni ule mfumo wa usafirishaji wa maandishi pamoja na picha katika websites,  na kazi yake kubwa ni kuangalia jinsi gani maandishi na picha yalivyotengenezwa na kuhakikisha inayasambaza kama ilivyo.

Mfano, unapoandika website katika browser ili uisome, hapo itatuma command ya HTTP ili ikachukue hiyo page uliyoiomba kuisoma kutoka kwa server yake na kukuletea katika browser yako kama ilivyo.

Hivyo hiyo ndiyo maana ya HTTP. Ila unaweza kujiuliza, mbona hatuandiki http tukiandika website fulani? Yaani kama unataka kusoma website kama google.com huna haja ya kuandika http lakini website hiyo itafunguka, je? Hiyo ina maana http haifanyi kazi hapo?

Jibu ni kwamba, huwezi kutembelea tovuti yoyote ile bila ya kutumia Browsers yaani (Internet Explorer, Mozilla Firefox, Safari, Google chrome n.k), hizo browsers zimetengenezwa kwa lengo hilo tu, hivyo katika sehemu ambayo unaandika address ya tovuti fulani tayari kuna Code zilishawekwa kabla ambazo zinaamuru kuwa, kila unachoandika katika sehemu hiyo kinaanziwa na http:// hata kama hujaandika.

Mfano huo unafanana na mfano wa namba ya mtihani ya mwanafunzi fulani, ukiulizwa na mwalimu wako namba yako ni ngapi, unaweza tu kumwambia ni 90, hapo mwalimu tayari ameshakuelewa kwani namba zote huanza na namba ya shule kwanza kisha ndiyo namba yako mfano, ikiwa namba ya shule ni S0111 hivyo namba yako kamili itakuwa S0111/90. Lakini ukiulizwa nje ya shule namba yako, ni lazima uanze na namba ya shule kwanza kisha ndiyo utaje ya kwako kwani aliyekuuliza siyo muhusika wa shule uliyotoka hivyo hawezi kufahamu namba ya shule yako.

Hivyo kwa mfano huo hapo juu, shule ndiyo mfano wa Browser, na tovuti ni mfano wa nambari ya mwanafunzi na http ni mfano wa nambari ya shule. Hivyo kuandika tovuti sehemu nyingine tofauti na Browser ni lazima uanze na http:// kisha ufatie na address ya tovuti unayohitaji kwani sehemu tofauti na Browser haitatambua address yako.

Jaribu mifano ifuatayo ili upate uelewa zaidi:

  1. Fungua browser yoyote (Internet Explorer, Mozilla Firefox, Safari, Google chrome n.k), kisha andika anwani ya tovuti yoyote ile mfano staryte.ucoz.com bila kuanza na http kama nilivyoiandika hapo. Hapo itafunguka.
  2. Fungua browser yoyote (Internet Explorer, Mozilla Firefox, Safari, Google chrome n.k), kisha andika anwani ya tovuti yoyote lakini anza na http:// mfano http://staryte.ucoz.com. Hapo itafunguka pia.
  3. Fungua Windows Explorer yoyote ile (My Computer, My Document, Local Disk C n.k) kisha andika anwani ya tovuti yoyote ile mfano staryte.ucoz.com bila kuanza na http kama nilivyoiandika hapo. Hapo haitafunguka. Note: katika windows explorer anwani huandikwa sehemu karibia na juu, utaona tu sehemu inayokuruhusu kuandika kitu. Angalia picha hapo chini:


     4.Fungua Windows Explorer yoyote ile (My Computer, My Document, Local Disk C n.k) kisha andika anwani ya tovuti yoyote lakini anza na http:// mfano http://staryte.ucoz.com. Hapo itafunguka lakini haitafunguka katika Windows Explorer bali itapeleka Command kwa Default Browser kisha itafungukia huko.

Tumeona katika jaribio la 3 kuwa, kwa vile Windows Explorer sio kazi yake kufungua na kuonyesha Tovuti hivyo kwa kuandika anwani bila ya http imeshindwa kutambua ni anwani ya aina gani.

Lakini katika jaribio la 4, kwa kuwa tulianza na kuandika http, hivyo Windows Explorer iliweza kutambua kuwa hiyo anwani ni ya tovuti fulani, hivyo basi, kwakuwa yenyewe kazi yake sio ya kuonyesha kurasa za website, hivyo ilipeleka command katika program inayohusika (browser) na hivyo tovuti hiyo kufunguka katika hiyo program husika.

Anwani zinazoweza kufunguliwa na Windows Explorer huanza kuandikwa na herufi ya Disk unayotaka kufungua ikifuatiwana jina la folder husika mfano, C:\ au D:\  kama unahitaji kuona faili zilizopo ndani  ya folder lilipewa jina la picha ambalo liko katika Disk F kwa mfano, utaandika F:\picha…. Hapo utaletewa mafaili yote yaliyo ndani ya folder la picha.

Kumbuka kuwa, Windows Explorer iliposhindwa kufungua website pale ulipoweka address sahihi ilipeleka taarifa kwenye program husika na hivyo address yako ikafunguka katika program husika yaani Browser (Internet Explorer, Mozilla Firefox, Safari, Google chrome n.k), vilevile katika Internet Explorer (IE), ukiandika address inayohusika na kufunguliwa na Windows Explorer mfano C:\ au D:\ basi itafanya vilevile kupeleka taarifa katika program husika na kuifungua address hiyo. Lakini kwa wanaotumia Mozilla Firefox, hiyo ina uwezo wa kufungua address za Windows Explorer ilimradi tu uwe umeandika address sahihi. Angalia picha hapo chini:


Ikiwa hakuna drive yenye herufi D halafu ukaandika address yake ili kufungua, hapo utapokea message ya makosa ikisema "Please insert Disk into Drive D” or "not found” au message yoyote ile kulingana na browser unayotumia.

Hayo ni maelezo yanayohusika na jinsi gani http inavyokuwa na umuhimu katika kuifanya address ijulikane kuwa ni tovuti, kumbuka kuwa ukijua jinsi ya kuzitumia address basi hutapata tabu ya kutafuta kitu katika computer yako ilimradi tu ujue jina lake.

NOTE: Majaribio ya kufungua tovuti yanahitaji uwe una connection na internet.

Ikiwa una swali lolote juu ya mada hii, au una tatizo katika suala zima la computer, usisite kutuuliza ili tukusaidie, tembelea ukurasa wa maswali na majibu kuuliza maswali yoyote uliyo nayo. Ahsante.

Category: COMPUTER | Added by: Admin (17/Jun/2013) | Author: Yahyou M. Yahya E W
Views: 1470 | Tags: Internet, website, elimu, kazi, jinsi, http, Computer, tovuti | Rating: 2.0/1
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: