[ New messages · Members · Forum rules · Search · RSS ]
  • Page 1 of 1
  • 1
Members msinichoke kwa maswali
seifDate: Thursday, 25/Jul/2013, 12:43 | Message # 1
Lieutenant
Messages: 42
Awards: 0
Reputation: 0
Status: Offline
Habari yenu wana Staryte, swali langu ni kwamba je kuna tatizo ukichomoa removable drive kama vile flash disk au moderm katika computer bila ya kubofya safe remove? na kama kuna tatizo je madhara yake ni yapi?

Yes I can
 
badshahDate: Thursday, 25/Jul/2013, 12:51 | Message # 2
Lieutenant
Messages: 59
Awards: 2
Reputation: 1
Status: Offline
from my side of things naweza kusema kwamba, kuchomoa flsh bila ya kuselect safe remove kuna madhara na pia hakuna madhara kwa sababu zifuatazo:

kuna madhara endapo flash itakuwa inatumika kama vile kukopi data au kuna window iko open inayoonyesha mafaili yaliyo ndani ya flash hiyo, na madhara yake unaweza kuifanya isifanye kazi baadaye au ikawa inafanya kazi lakini kwa kiwango cha chini kabisa na ndio maana utaona baadhi ya flash ziko slow sana katika kukopi data hata ndogo ndogo. na pia madhara yanaweza pia yasitokee katika flash peke yake bali hata katika ile port ya computer ya kuchomekea hiyo flsh inaweza kufa na isifanye kazi.

lakini ikiwa flash umeichomeka katika computer na hakuna kazi yoyote ile inayoendelea katika flash hiyo, basi ukiichomoa bila ya kutumia safe remove haiwezi kuathiri kitu chochote, ila unasisitizwa sana utumie safe remove kwani siku hizi kuna virus ambao huifanya flash iwe busy hata kama huitumii kwa muda huo hivyo ili kuepuka madhara hayo ya kutokujua ni bora tu utumie safe remove. Obrigado!
 
Miss_NeeluDate: Thursday, 25/Jul/2013, 12:53 | Message # 3
Sergeant
Messages: 26
Awards: 0
Reputation: 1
Status: Offline
Thanks Hassan, for this question and thanks a lot Badshah, for your answer tumeelimika wengi kwa hili
 
seifDate: Thursday, 25/Jul/2013, 12:55 | Message # 4
Lieutenant
Messages: 42
Awards: 0
Reputation: 0
Status: Offline
thanks Badshah, nimekuelewa tena sana... kumbe virus wanaweza kufanya flash ikawa busy? na huwa inatokea vipi? sorry lakini

Yes I can
 
badshahDate: Thursday, 25/Jul/2013, 13:01 | Message # 5
Lieutenant
Messages: 59
Awards: 2
Reputation: 1
Status: Offline
yeah Hassan, wanaweza kufanya hivyo kwani siku zote Virus wana kazi ya kuharibu na si kutengeneza, na sio kwamba huko kuwa busy kunafanyika kwa kuingizza data au kitu kingine hapana basi tu ilimradi kuleta vurugu, na ndio maana kuna wakati utaona ile taa ya kwenye flash inawakawaka kwa kublink utadhani kuna data zinakopiwa na hali ya kuwa hakuna data inayokopiwa.au sometimes utaona ukiclick safe remove inakuja message ikikwambia "the device is currently in use" na hali ya kuwa huitumii kwa lolote.
 
  • Page 1 of 1
  • 1
Search: