Jamaa alipata urithi wa shilingi milioni 20, kwa kuzihifadhialiona ni bora aende sehemu azifukie chini. Basi akaenda mbali sana mpaka sehemu moja, kisha akachimba shimo chini ya mti mmoja hivi na kuzifukia zile fedha zote humo. Ili asipoteze kumbukumbu ya mahali hapo ikabidi arudi hatua kama 10 hivi na kupiga picha ule mti ili aukumbuke pale atakapohitaji fedha zake. Basi aliporudi nyumbani kwake akaitazama ile picha aliyopiga, mara akashituka sana kuona juu ya ule mti kuna mtu alikuwepo tena akiwa anachekelea sana.