Home » Articles » COMPUTER

JINSI YA KUIFANYA COMPUTER YAKO KUWA NA ULINZI MZURI

JINSI YA KUIFANYA COMPUTER YAKO KUWA NA ULINZI MZURI


Katika upande huu tutaangalia jinsi gani unaweza kudumu na system yako ikiwa inafanya kazi kwa ufanisi hali ya kukufurahisha. Mara nyingi compyuta ambazo hazina ulinzi hufanya kazi kwa tabu sana na hata kumkatisha tamaa mtumiaji na hali ya kuwa computer hiyo ina ukubwa mzuri wa RAM na Processor yake ina speed ya kuridhisha. hali hii hutokea endapo system yako imevamiwa na program zinazotengenezwa kuharibu mfumo mzima wa utendaji kazi wa computer. zifuatazo nio njia nzuri kabisa za kuondokana na tatizo hili.

Angalia kama una antivirus katika kompyuta yako. Kompyuta nyingi (Desktop na Laptops) huja pamoja na Antivirus pamoja. Hata hivyo, kuna wakati inawezekana ulinzi ukawa hautoshelezi, hivyo kulazimika kulipia huduma ya Antivirus ambazo zinakusaidia kulinda kompyuta yako. Antivirus ambayo ni nzuri na ni ya bure ni AVG (AVG free Edition), ambayo unaweza kuidownload katika tovuti ya www.download.com.


Angalia kama Windows Defender yako inafanya kazi. Nenda katika Control Panel halafu bofya  System and Security. Kama hauna basi hutaona neno kama hilo, funga hiyo Control Panel. au kwa njia nyingine ya kutafuta nenda Start menu (inapatika chini kushoto kwa asilimia kubwa ya kompyuta ikiwa mtumiaji hatabadilisha) halafu sehemu ya Search Box andika neno ""Windows Defender.” Kama hakuna matokeo yoyote basi ujue hauna kitu kama hicho hivyo unatakiwa ukidownload hapa http://www.microsoft.com/download/en/details.aspx?id=17. Baada ya kudownload, ifungue. Iwashe (turn it on), halafu iache ifanye scanning ya kompyuta nzima mara ya kwanza. Ikishamaliza basi itaanza kulinda kompyuta yako kutokana na program zisizotakiwa na zenye madhara.


Angalia kama Windows Firewall yako iko on.

Anza Start halafu nenda kwende Control Panel kisha utaona neno Windows Firewall.  Hakikisha iko on, na utaona pia pembeni ya neno "On” kuna maneno yako ndani ya mabano yameandikwa "(Recommended)” ikiwa na maana kuwa imesisitizwa kuwekwa on kuliko kuwekwa Off. angali picha hapa chini:-

 


Update Windows yako.

Hakikisha una Update windows yako ili kuweza kuwa katika usalama zaidi. Ili usipate tabu ya kufanya hivi basi ni vizuri kuweka Automatic Updates kuwa on.  Kuweka Automatic Updates on  fuata hivi:-

Start >> Controll Panel >> Automatic Updates .angalia picha yake hapa chini:-


 

Download kitu kinachoitwa SpyBot Search and Destroy.

Software  hii itakusaidia ku-scan system yako nzima na kuondoa kila program mbaya ambazo hazitakiwi katika kompyuta yako. Unaweza kudownload software hii kwenye www.download.com.

 

 

Muhimu:

  • Kuona kama kweli uko katika ulinzi mzuri kutokana na program au vitu vinavyoweza kukuharibia kompyuta yako, nenda www.grc.com na iache ijaribu system yako. Kama itaingia ndani ya system yako basi jua kwamba Firewall yako haifanyi kazi na inabidi udownload nyingine. Lakini kama itakuletea ujumbe kama huu "all ports are closed or in stealth mode” basi Hongera!! Uko katika ulinzi mzuri wa system yako.
  • Siku zote ni vizuri na ni wazo zuri ku download ulinzi wa Spyware (Antispyware) zaidi ya moja lakini si antivirus au firewalls.



Onyo:

  • Ingawa kuna antivirus nyingi zitolewazo bure, lakini install moja tu. Ukiweka zaidi ya moja basi utasababisha kuchanganyikiwa kwa ufanyaji kazi wa program zako za ulinzi wa virus.
  • Kama uki install firewall nyingine tofauti na ile iliyoko katika Windows, basi izime hiyo Windows Firewall (turn off Windows Firewall). Usiache firewall mbili zikafanya kazi kwa wakati mmoja.

Natumaini umepata kilicho bora katika suala zima za ulinzi wa system yako.



Category: COMPUTER | Added by: Admin (22/Mar/2013)
Views: 3221 | Tags: Spyware, system, Windows, Firewall, Computer, ulinzi, anti virus | Rating: 2.5/2
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: