Home » Articles » EDUCATION

FAHAMU HISTORIA YA KATUNI MAARUFU YA TOM & JERRY

FAHAMU HISTORIA YA KATUNI MAARUFU YA TOM & JERRY


Tom & Jerry ni katuni inayoongoza kwa kupendwa sana hapa ulimwenguni, hata watu wazima hukaa na kuangalia katuni hii na imejipatia umaarufu mkubwa sana mpaka leo hii.

Katuni hii ilianzishwa na mmarekani  ajulikanaye kama Fred Quimby ambaye kwa sasa ni marehemu, Fred Quimby alifariki mwaka 1955. Mtunzi huyu alijitahidi sana katika utengenezaji wa katuni hawa kuanzia mwaka 1918 Hadi 1955 akiwa katika studio za animation Metro Goldwyn Mayor (MGM) Ambaye alikuwa akitengeneza katuni hawa kwa vipande vipande vya video vilivyokuwa vikichukua urefu wa dakika 5 hadi 8 kwa kila kipande.

Utaona kuwa hata mazingira ya katuni hawa wa Fred Quimby yanafanana na maizingira halisi ya wakati huo. Mfano ukiangalia katuni za Fred Quimby utaona wakitumia redio za kizamani au player (inatumia rekodi kama sahani hivi na mkono mmoja mfano wake ni kama zile zitumiwazo na ma DJ) ambazo kwa sasa hata madukani huwezi kuzikuta. Kipindi hicho kulikuwa hakuna redio za CD hivyo huwezi kuona Tom au Jerry akitumia Redio za CD wakati huo.

 

Baada ya kufariki Fred Quimby, alitokea mtunzi mwingine aliyejulikana kwa jina la Chuck Jones ambaye alikuwa hapo kabla akitengeneza katuni mbalimbali kama vile za sungura n.k. alianza kutengeneza na kuendeleza katuni hawa kuanzia mwaka 1963 hadi 1967. Chuck Jones alifariki mwaka 2002. Muonekano wa katuni hawa unatofautiana sana, kama ukiwaangalia kwa makini utagundua kuwa Tom wa Fred Quimby hafanani kabisa na Tom wa Chuck Jones na hata mazingira yao ni tofauti kulingana na wakati wao. Mazingira ya Chuck Jones  yanaonekana kuwa na maendeleo zaidi kuliko ya Fred Quimby.

 

Katuni hii ya Tom & Jerry haikukosa waendelezaji kwani iliendelea kutengenezwa na studio za Wanna Bros na mpaka sasa inaendelea kutengenezwa na kuonyeshwa katika channel za katuni kama vile Cartoon Netwrok (CN) na Boomerang ikijulikana kama Tom & Jerry the tales. Hata ukitafuta katika Youtube unazikuta nyingi tu, na utagundua tofauti yao kulingana na mazingira ya wakati ambao katuni hizo zimetengenezwa. Katuni hii ina wapenzi wengi sana ulimwenguni kwa rika lote yaani hata watu wazima hufurahi sana wanapoangalia katuni hii.

 

Category: EDUCATION | Added by: Admin (05/Jul/2013) | Author: Yahyou M. Yahya E W
Views: 2368 | Rating: 1.8/5
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: