Home » Articles » HEALTH

BAADHI YA MARADHI YANAYOWEZA KUONDOKA KWA KUTUMIA KITUNGUU THAUMU.

BAADHI YA MARADHI YANAYOWEZA KUONDOKA KWA KUTUMIA KITUNGUU THAUMU.


Uziwi (kutosikia)

Kuna tatizo hili kwa baadhi ya watu kuwa na uwezo mdogo sana wa kusikia au kutosikia kabisa ingawa sio viziwi wala hawajazaliwa na tatizo hili bali ni hali iliyowatokea ukubwani. Ponda tembe saba za thaumu kasha utie katika mafuta ya zeti (Olive Oil) kisha uweke juu ya moto mdogo, mafuta yakishapata moto (sio ya kuunguza) tia sikioni kadiri ya matone machache kwa kutumia pamba safi, usitoe mpaka asubuhi, na utatia siku moja na ya pili usitie fanya hivyo hivyo mpaka utapata nafuu.

 

Mafua

Meza tembe moja ya thaumu baada ya chakula na unywe juice yake iliyochanganywa na ndimu na pia ukiichoma kwa kujifukiza ni dawa nzuri sana ya kuondoa mafua.

 

Cholera (kipindupindu)

Ugonjwa huu ni wa mlipuko hivyo ukijua kwamba katika eneo lako unaloishi tayari ugonjwa huu umeanza kushambulia basi kinga yake ni kama ifuatavyo kwa kutumia thaumu. Chukua thaumu uifanye laini kwa kuisaga, ichanganye na asali kisha ule kila unapomaliza kula chakula ni kinga nzuri sana.

 

Kutoa wadudu tumboni

Ponda tembe tatu za thaumu utie katika maziwa, unywe bila kutia sukari kabla ya kulala. Ukiendelea hivi kwa muda mfupi tu utasafishika tumbo kwa kuondoa wadudu wote tumboni ambao kwa njia moja au nyingine huwa ni vyanzo mbalimbali vya maradhi ya tumbo.

 

Blood Pressure

Hili ni tatizo sugu sana kwa asilimia kubwa ya watu sasa, ukila tembe moja ya thaumu kabla ya kunywa chai asubuhi (Breakfast) kila siku huzuia kupata shinikizo la damu ya kupanda (High Blood Pressure) na hutoa cholestral (Lehemu) katika damu, na thaumu si kwaajili ya kuzuia Presha kupanda tu bali pia huondoa cholestral katika damu na kufanya moyo kufanya kazi yake vizuri ikatembea mwilini kwa urahisi.

 

Unaweza kuwa na swali cholestral ni nini? Haya ni mafuta ya ndani ya damu, hufanya damu kuwa nzito na mishipa kugandana na mafuta. Na vyakula vyenye cholestral ni kama vile Nyama ya ng’ome, mbuzi, kondoo (nyama nyekundu zote). Nyama nzuri ni nyama nyeupe  nayo ni nyama ya kuku, samaki wadogo, lakini  maziwa full cream, mayai, viazi, samli safi, siagi, hizi zina cholestral nyingi. Na vyakula vyenye cholestral ni vibaya kwa wenye maradhi ya moyo na presha, lakini hata ambaye hana maradhi hayo si vema kutumia vyakula hivyo kwa sana, hivyo inafaa apunguze kutumia hivyo, lakini vipo vyakula au dawa zinazotoa cholestral kama hiyo thaumu.

 

Unaweza kuchangia au kutoa maoni yako katika kisanduku hapo chini.

Category: HEALTH | Added by: Admin (01/May/2013)
Views: 3786 | Tags: saumu, faida, kitunguu, maradhi, tiba, thomu, thaumu | Rating: 1.4/7
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: