Home » Articles » HEALTH

DHANA YA UKEKETAJI

DHANA YA UKEKETAJI


Ni moja ya tatizo sugu sana linalowakabili wanawake katika jamii nyingi. Imekadiriwa ulimwengu mzima kuwa wanawake takriban milioni 120 wamekumbwa na tatizo hili.

Wanaounga mkono ukeketaji husema kuwa ni sehemu muhimu sana katika maisha ya kiutamaduni na kidini, na wengine hulinganisha na ile hali ya kutahiriwa mwanaume ambayo haipingwi hata kidogo na ni halali.

Lakini wale wanaopinga dhana ya ukeketaji husema kwamba, sio tu kwamba ukeketaji hutishia maisha ya wanawake, bali pia ni moja ya njia za unyanyasaji wa wanawake.

Katika baadhi ya nchi ambazo ukeketaji hufanyika sana utakuta ni kinyume na sheria – wale wanaong’ang’ania kufanya uchafu huu katika nchi hizo sasa wanaweza kushitakiwa na kufungwa, lakini bado hufanyika kimya kimya ndani ya familia na mbali na macho ya vyombo vya sheria.

Ukeketaji hufanyika sehemu kubwa magharibi na kusini mwa Asia, Afrika ya kati na Mashariki na sehemu nyingi za Afrika. Pia huonekana kufanyika baina ya wahamiaji katika nchi ya USA, Canada, France, Australia and Britain, mahali ambapo ni kinyume na sheria. Kwa ujumla imekadiriwa kuwa zaidi ya wasichana milioni 2 hukeketwa ndani ya mwaka mmoja.

Kuna aina tofauti  za ukeketaji.

  1. Uondoaji wa ncha ya kisimi (The removal of the tip of the clitoris)
  2. Uondoaji wa Kisimi(clitoris) na Labia na ushonaji wa uke, kwa kuacha njia ndogo tu ya mkojo na damu ya hedhi. Mchakato huu hujulikana kama ufyataji (hali ya kufunga uke kwa bizimu/kushona kuzuia kujamiiana.) – Infibulation.

Hakuna faida yoyote ile ya kiafya isipokuwa ni madhara

Ukeketaji hauna faida za kiafya hata kidogo, na inawaathiri wanawake na wasichana katika njia nyingi sana. Inahusisha kuondoa na kuharibu sehemu na tezi muhimu katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na kuzuia utendaji kazi wa asili wa mwili.

Huweza kumsababishia maumivu makali, homa, mshtuko, uvujaji wa damu, ugonjwa wa pepopunda (tetanus), kufunga njia ya mkojo.

Pia humondolea hamu yakufanya tendo la ndoa.



Madhara ya muda mrefu ni kama yafuatayo:

  1. Maradhi ya mara kwa mara ya kibofu na njia za mkojo
  2. Uvimbe katika kibofu
  3. Ugumba
  4. Matatizo katika kujifungua hasa kumuua mtoto anayezaliwa kulingana na njia kubanwa na mishono ya ukeketwaji.

Ikiwa elimu ya hili itawafikia wahusika wa kazi hizi, na hatua kali za kisheria kuchukiliwa ipasavyo dhidi ya wanaounga mkono pamoja na kutenda, basi ukeketaji unaweza kumalizika kwa haraka kabisa.

 

Category: HEALTH | Added by: Admin (16/Jun/2013) | Author: Yahyou M. Yahya E W
Views: 2636 | Tags: madhara, afya, ukeketaji, maradhi, dhana | Rating: 2.0/1
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: