Home » Articles » HEALTH

Dondoo 5 kwa ngozi yenye Afya.

Dondoo 5 kwa ngozi yenye Afya.

Uangalizi mzuri wa Ngozi — ikiwemo kulinda ngozi na Mwanga wa Jua pamoja na kuiosha kwa utaratibu — itafanya ngozi yako kuwa na Afya na kuishi kwa ubora miaka yote.

Je? Hauna muda wa kuitunza ngozi yako? Jitahidi kufata misingi bora. Utunzaji wa ngozi yako na kujichagulia mfumo mzuri wa Afya katika maisha yako kunaweza kukusaidia kuchelewesha mchakato wa ngozi yako kuzeeka mapema na pia kulinda matatizo mbalimbali ya ngozi. Fuata hizi Dondoo tano (5).

1.   Jilinde kutokana na Jua.

Moja ya njia bora zaidi ambazo unatakiwa kuzifanya ni kulinda ngozi yako na mwanga wa Jua. Mwanga wa jua huweza kukusababishia mikunjo mikunjo, madoa madoa hasa ya uzee na matatizo mengine mengine ya ngozi – vilevile kuweza kukusababishia Saratani ya Ngozi.

Ulinzi bora zaidi wa jua katika ngozi yako ni kama ifuatavyo:

  1. Tafuta kivuli. Epuka mwanga wa Jua pale inapofikia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni, muda huu huwa jua linakuwa kali sana hivyo uwezekano wa kuathiri ngozi yako ni rahisi sana.

 

  1. Vaa nguo zenye kuilinda ngozi. Funika ngozi yako kwa shati ya mikono mirefu ya kitambaa kisichoruhusu joto (hasa nguo za kufuma), suruali ndefu na kofia yenye upana wa kuweza kuzuia mwanga wa jua hasa pale unapotoka nje au kwenda sehemu yoyote ile wakati mwanga wa jua ni mkali.

    2.   Usivute sigara.

          Uvutaji wa sigara hufanya ngozi yako kuzeeka na kutengeneza mikunjo. Uvutaji wa sigara hukondesha vishipa vidogo vipatikanavyo katika tabaka la juu ya ngozi, ambayo hupunguza upitishaji wa damu. Hali hii huinyima ngozi Oxygen na virutubisho muhimu. Uvutaji wa sigara pia huharibu vinyweleo ambavyo vinaipa ngozi nguvu na kuifanya iwe nyororo. Kwa nyongeza tu ni kwamba kile kitendo kinachoendelea endelea kila siku unachokifanya usoni pale unapovuta sigara, kama vile kutanua mashavu wakati wa kutoa au kuingiza moshi na kufinya finya macho hufanya ngozi ya uso kujikunja kwani mwili wa binadamu hujiweka vile unavyouzoesha.

            Kama unavuta sigara, basi njia bora ya kuilinda ngozi yako ni kuacha. Muombe daktari wako akupe dondoo na matibabu ya kukusaidia kuacha kuvuta sigara.


3.   Itunze ngozi yako kwa upole kabisa.

Uoshaji wa kila siku na kunyoa kunaweza kuharibu ngozi yako. Kuifanya nyororo fuata haya yafuatayo:

                      I.        Jaribu kupunguza muda wa  kuoga. Ninaposema hivi haina maana kuwa usioge, kuoga ni katika usafi na ni afya ila usikae muda mrefu bafuni. Maji ya moto na kuoga kwa muda mrefu huondoa mafuta katika ngozi yako, jitahidi kupunguza muda wa kukaa bafuni na tumia maji yaliyopoa ili kusaidia kuwa na afya katika ngozi yako.

 

                    II.        Epuka kutumia sabuni ngumu. Sabuni kama hizi au sabuni za dawa kali huondoa mafuta mafuta katika ngozi. Badala yake, tumia sabuni zilizo laini.

 

                   III.        Nyoa kwa uangalifu. Kulinda na kuifanya ngozi yako iwe na mafuta tumia Shaving Cream, losheni au Gel kabla ya kunyoa. Na kwa unyoaji wa kuondoa nywele kabisa kabisa tumia kiwembe kikali na hakikisha unanyoa kuelekea kule nywele au ndevu zinapoelekea na si kinyume chake.

 

                  IV.        Kausha. Baada ya kuosha au kuoga, kwa utaratibu kausha ngozi yako kwa kutumia taulo ili baadhi ya unyevu kubakia ndani ya ngozi.

 

                   V.        Lainisha ngozi kavu. Kama ngozi yako ni kavu, tumia dawa za kulainisha (moisturizer) ambayo inaendana na aina ya ngozi yako. Kwa matumizi ya kila siku, tumia moisturizer ambazo zima SPF. Ukitaka kununua jaribu kuulizia hili.

Daily cleansing and shaving can take a toll on your skin. To keep it gentle:

4.   Kula vyakula vyenye Afya.


Mlo kamili na wenye Afya bora husaidia kujiona vizuri na kujisikia vile utakavyo. Kula matunda sana, mboga za majani, nafaka nafaka pamoja na protini kidogo. Uhusiano baina ya mlo na chunusi hauko wazi – lakini baadhi ya utafiti unapendekeza kwamba mlo unaoleta vitamin C na wenye Fat kidogo na Carbohydrate iliyotengenezwa vizuri inaweza kufanya ngozi yako kuonekana mpya kila siku

5.   Jitahidi kuepuka mfadhaiko au mawazo.

Mawazo uliyoshindwa kuyakabili na kuyaondoa yanaweza yakafanya ngozi yako kuwa na urahisi wa kutokeza chunusi na matatizo mengine. Kuboresha  Afya ya ngozi yako na hali ya fikra ya afya yako – chukua hatua za kuzuia mawazo. Tengeneza njia za kukuwezesha kuzuia hili, tengeneza ratiba ya kufanya vitu ambavyo unafurahia kuvifanya na usikae peke yako bila kazi yoyote. Matokeo yake yanaweza kuonekana kama ndoto kuliko ulivyotegemea.

Ni tumaini langu kuwa umefurahia dondoo hizi chache ambazo ukuzifuata zinaweza kukusaidia katika kuboresha Afya ya Ngozi yako. Ikiwa una la ziada, jisikie huru kuacha maoni yako hapa ili sote tunufaike katika kuelimishana juu ya jambo hili.

Nakutakia kila la kheri katika kutafute kile bora unachohitaji.


Category: HEALTH | Added by: Admin (27/Mar/2013) E W
Views: 3425 | Comments: 2 | Tags: ngozi, Skin, chunusi, tunza, Health, uso | Rating: 1.0/3
Total comments: 2
1 ameer  
0 Spam
nashkuru kwa dondoo zenu naomba mzidi kutuletea mengi zaidi

2 Admin  
0 Spam
You are most Welcome

Name *:
Email *:
Code *: