Home » Articles » HEALTH |
KITUNGUU HUPONYA YALIYOSHINDIKANA maradhi mengi hutibika kwa kutumia juisi ya kitunguu. Katika makala ya leo nawaeleza faida za juisi ya kitunguu maji katika mwili wako, ikiwemo uwezo wake wa kuzuia na kutibu magonjwa sugu na yaliyoshindikana kwa kutumia dawa za hospitali.
Tunapaswa kutambua kwamba viungo vingi tunavyotumia jikoni kwenye vyakula vyetu kila siku vina uwezo mkubwa wa kuponya magonjwa yanayotusumbua. sina shaka kama kuna mtu ambaye hakijui kitunguu, nyanya au kitunguu saumu. Kitunguu maji ni kiungo cha mboga, ambacho aghalabu hutumika katika mapishi ili kuongeza ladha katika chakula na wakati mwingine hutumika kutengenezea kachumbari kwa kutokujua umuhimu wake mwilini.
KITUNGUU KINATIBU YAFUATAYO Katika orodha ndefu ya magonjwa yanayotibika PASIPO SHAKA kwa kutumia juisi ya kitunguu, ni pamoja na ugonjwa unaowasumbua watu wengi wa kutokwa na damu sehemu ya haja kubwa wakati wa kujisaidia.
Ugonjwa huu, ambao kwa kitaalamu unajulikana kama `Hemorrhoids’ au `Piles’ unawatokea watu wengi ambao kama mtu hakupata nafuu kwa kula vidonge, suluhisho la mwisho huwa ni kufanyiwa upasuaji mdogo katika njia ya haja kubwa, upasuaji ambao huambatana na maumivu makali. Kwa wale ambao wameshakutwa na tatizo hili au wanalo hadi sasa, dawa kama vile ANUL SUPPOSITORIES, SECNIDAZOL, n.k. zinajulikana sana kwao kwa sababu ndiyo dawa zinazopendekezwa na madaktari wengi kutumiwa ili kutibu PILES. Unaweza ukapona kwa muda na tatizo likajirudia baadaye au unaweza usipone na ukalazimika kufanyiwa upasuaji.
Lakini kwa kutumia juisi ya kitunguu, unaweza ukapona kabisa na inawezekana tatizo lisijirudie, kwani mzizi wa tatizo huondoka kabisa kutoka tumboni.
SIFA YA KITUNGUU Kitunguu kina virutubisho vyenye uwezo wa kuua bakteria (antibacterial) na fagasi mwilini (anti fungus). Pia kina virutubisho vyenye uwezo wa kuzuia wanaosababisha magonjwa nyemelezi (anti free radicals) na magonjwa ya viumbe (anti informatory). Mbali na sifa hizo , kitunguu kina kiwango kikubwa cha madini kama vile `calcium’, `magnesium’, `sodium’, `potassium’, `selenium’, `phosphorus’, na bila kusahau kiasi kidogo cha aina fulani ya mafuta ambayo huimarisha kinga ya mwili.
JINSI YA KUJITIBU `HEMORRHOIDS’. Kama nilivyoanza kusema awali, pamoja na magonjwa mengine yanayotibika kwa kitunguu, leo tutaanza kwanza na ugonjwa huu unaosumbua watu wengi. Dawa hii ni ya uhakika kwa mtu atakayeweza kuitumia kama inavyotakiwa.
Kunywa juisi ya kitunguu kila siku asubuhi kwa muda wa siku saba hadi siku 14, ikitegemea na ukubwa wa tatizo lako. Juisi hiyo lazima uinywe asubuhi kabla ya kula kitu chochote (on empty stomach) na utaruhusiwa kunywa kifungua kinywa chako saa moja baada ya kunywa juisi hiyo. Dozi hii ni maalumu kwa ajili ya kutibu `hemorrhoids’, ingawa wakati ukitibu tatizo, matatizo mengine yaliyomo mwili yatakuwa yakijiondoa. Napenda kuhakikisha kuwa tiba hii ni ya uhakika na haina madhara yoyote.
TAHADHARI Mara baada ya kuinywa juisi hii kwa mara ya kwanza na siku chache zitakazofuata, utajisikia vibaya na tumbo kuchafuka. Hali hii na ya kawaida, unachotakiwa kufanya mara baada ya kunywa, ni kukaa au kulala kwa muda , baada ya muda hali yako itarejea kama kawaida. Baada ya siku tatu, ukinywa mwili utaizoea na utajisikia kawaida tu.
Katika makala ifuatayo tutaangalia maradhi mengine yanayoweza kutibika kwa kitunguu na kuona jinsi ya kutengeneza juisi yake. | |
Views: 2978 | | |
Total comments: 0 | |