Home » Articles » HEALTH

VIATU VYENYE VISIGINO VIREFU

VIATU VYENYE VISIGINO VIREFU

Sababu ya kwanini usivae viatu hivi


Kuna sababu za msingi kabisa za kuacha kuvaa viatu vya visigino virefu au kama si hivyo bali ni kupunguza muda wa kuvivaa. Hakika vinaonekana vizuri na kuvutia na wanawake wengi hupenda sana. Hata hivyo, haiwi vema kulazimisha miguu yako kunyanyuka inchi 4 mpaka 5 muda wote. Kama unafanya hivi basi utakuja kuona matatizo yake baadaye. Hizi ni baadhi ya sababu za msingi kabisa za kuacha kuvaa viatu hivi.

 

  1. kutembea

moja ya sababu yenye kuleta akili ni hii hali ya kutembea. Endapo utatembea mwendo mrefu. Jaribu kufikiria kuwa wewe uliyevaa viatu hivi vya visigino virefu na yule aliyevaa vifupi nani atatembea vizuri na kwa raha zaidi? Hivyo epuka kuvaa hivi na kama miguu ingekuwa na uwezo wa kuongea basi ingekushukuru sana ukiivalisha viatu vyenye soli yenye kulingana urefu.

 

  1. kuumia

unaweza kutembea katika njia ambayo haiko sawasawa labda ina mashimo, au mabonde au hata kama imenyooka lakini mara nyingi kulingana na uzito wa mtu kuna ukosefu wa balance unapatikana hapo hivyo ni rahisi sana kujitega na unaweza kuumiza viungio vya miguu yako.

 

  1. Kushindwa kuendesha (gari/pikipiki n.k.)

Viatu hivi havitakuruhusu kuendesha gari au pikipiki au kitu chochote kwa faraja, na inaweza kukuharibia uwezo na ufanisi wako katika udereva. Kama unaendesha kuelekea sehemu ambayo unahitaji kuvaa viatu vizuri basi vipo viatu vizuri vyenye kuvutia ambavyo viko flat chini. Kwa mwendo huo, unaweza kuendesha kwa usalama na ukaonekana vizuri tu.

 

  1. Usalama

Dunia hii hukumbwa na machafuko mengi sana na vilevile hujui machafuko yanaweza kutokea lini na saa ngapi. Endapo utakutana na tatizo ambalo litahitaji wewe kuondoka sehemu ulipo kwa haraka basi kukimbia hali ya kuwa umevaa viatu virefu haitawezekana. Hivyo kwa ajili ya usalama ni vema uvae viatu vifupi hasa ikiwa unajua muda wako wa kurudi ni usiku wakati ambao machafuko au balaa hutokea kwa asilimia kubwa.

 

  1. Afya

Kwa hakika viatu vyenye visigino virefu vinavutia sana, na vinafanya miguu yako kuonekana vizuri mno. Lakini je ni jambo la thamani kuumiza miguu yako kwa ajili ya urembo? Hatuko makini sana na miguu yetu na ndio maana tunafanya vile tunavyojisikia lakini ukweli ni kwamba mguu kunyanyuka kwa muda mrefu unaumiza viungio vyake na baadaye sasa ndio utakuta mtu hupata matatizo kama vile malengelenge, sugu na ngozi kuwa kama iliyoungua.

 

  1. Urefu

Mtu hufikiri kwamba viatu hivi hutufanya tuonekane warefu. Kwa bahati mbaya tunajidanganya, haileti maana kabisa kusema kuwa nchi 4 zinaweza kutuongezea urefu na pia hebu fikiria jambo moja unatakaje kuwa mrefu wa muda? Mara unaonekana mrefu kesho usipovaa utaonekana mfupi, na najua ya kwamba hatuvai au kupendeza kwa nafsi zetu bali hata kuwapendezeshea wengine sasa huyo nani utakayemdanganya urefu huo hali ya kuwa anakuona uko juu ya kitu? Hivyo ni vema kuutumia urefu uliokadiriwa na mungu vizuri hata ukazoeleka nao kwani urefu wa asili haubadiliki hata ufanye nini.

 

Hakuna sababu (labda uwe umeumia) ya kwamba huwezi kuvaa viatu hivi katika sherehe. Vinaonekana vizuri, vinapendeza na kukufanya uvutie na kujisikia vizuri katika sherehe. Hata hivyo kwa hayo yote tuliyoyaeleza hapo juu, viatu vya visigino virefu havifai kwa kuvivaa kila mara. Vitunze kwaajili ya sherehe maalum na utunze miguu yako.

 

Kwa maswali maoni au ushauri, jisikie huru kutuandikia katika kisanduku hapo chini.

 

Category: HEALTH | Added by: Admin (11/May/2013)
Views: 1631 | Tags: tatizo, refu, matatizo, sherehe, tabu, visigino, viatu | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: