Home » Articles » HEALTH

Vinavyoweza kusababisha PUMU, Fahamu Njia bora ya kujikinga na Kisukari

Vinavyoweza kusababisha PUMU, Fahamu Njia bora ya kujikinga na Kisukari

 

JIHADHARI NA VYENYE KUSABABISHA PUMU:

 

  1. Manyoya ya wanyama kama vile paka, Mbwa, N.k.
  2. Sigara, ile hali ya kuvuta na kutoa moshi ndani ya mapafu.
  3. Moshi, kama vile moshi wa kuni au wa takataka zinapochomwa.
  4. Vumbi, kama vile la kitanda au mto unapoukung’uta au hata unapofagia.
  5. harufu kali za Spray kama dawa za mbu N.K.
  6. mauwa yenye harufu kali kama vile mlangilangi, viluwa, yasmini n.k
  7. Hali ya hewa (weather)
  8. manukato au pafyum zenye harufu kali kama vile shampoo, sabuni, lotion N.K.
  9. kukimbia sana hasa kwa kwenda dhidi ya muelekeo wa upepo (against wind direction)

 

Pumu huweza kumshika mtu ukubwani na hata uzeeni huweza ikakushambulia.

 

DIABETES (Kisukari)


Kuna maradhi haya ya Diabetes. Medical writer mmoja wa Washington (U.S.A) ambaye ameandika kwamba watu wenye hofu au hatari ya kupata diabetes wanaweza kuondosha nusu ya hofu yao kwa kufanya mazoezi ya kutembea kwa muda wa dakika 30 kila siku na kupunguza uzito wa mwili wao.

 

Kutumia dawa inayoitwa METFORMIN pia huondosha hatari ya kupata Diabetes kidogo kidogo lakini si kama kutumia vyakula maalum, lakini lililo bora zaidi ni kufanya mazoezi (Body Exercise).

 

Hii ni mara ya kwanza kuwa dawa ya Diabetes kuthibitishwa kuwa ni kinga. Madakatari wengi wameshauri kupunguza uzito wa mwili lakini hawakuthibitisha wapunguze uzito kadiri gani na mazoezi pia yanahitajiwa hasa kwa kutembea kwa miguu, wala hawahitaji mbio kali kama za marathon au kujiweka na njaa.

 

Kwa mwendo wa dakika 30 kila siku si jambo gumu amesema daktari specialist wa Massachusetts General Hospital.

 

Na baada ya umri wa miaka 40 huwa iko hatari kila umri ukienda mbele ingawaje watoto ambao ni wanene (unene ulio zaidi ya umri wao) pia huwezekana kupata Diabetes.

 

Kuna hatari kubwa ya watu wasiofanya mazoezi ya mwili kupata Diabetes na hasa wale wanaokula sana huku wakitembea kwa magari au pikipiki bila hata kutenga muda wa kutembea kwa miguu japo dakika 30 kama tulivyoelezea hapo juu.

 

Changia hoja yako au kwa maswali na ushauri toa maoni katika kisanduku hapo chini.

Category: HEALTH | Added by: Admin (06/May/2013)
Views: 1162 | Tags: vumbi. mazoezi, body, diabetes, pumu, kisukari | Rating: 0.0/0
Total comments: 0
Name *:
Email *:
Code *: