Home » Articles » HEALTH |
WASIA WA MATABIBU(MADAKTARI) Kuna mambo mbalimbali ambayo watu wengi sana katika jamii yetu hii ya leo hawayafahamu, au huyachukulia ni mambo ya kawaida sana na kumbe yana madhara kiafya. Katika makala ya leo hii nimejaribu kupitia sehemu mbalimbali ili kuwaletea kile kilicho bora kama ushauri wa kufuata ili kuboresha afya yako, na makala yangu hii ya leo nimeamua kuwaandikia wasia wa matatibu mbalimbali katika kulinda afya yako. Hebu tuangalie ni wasia upi huo? Wasia wa kwanza: si vema mtu kula samaki pamoja na mayai kwa wakati mmoja. Na mtu akifanya hivyo ana asilimia kubwa sana ya kupata ugonjwa wa kupooza viungo au kiharusi. Wasia wa pili: si vema mtu kula samaki pamoja na maziwa kwa wakati mmoja. Na mtu akifanya hivyo ana hatihati ya kupata maradhi ya ukoma au mbaranga. Wasia wa tatu: ikiwa umeota ndoto za kimapenzi kisha ukatokwa na manii, halafu ukamuingilia mkeo bila ya kuoga, basi ana asilimia kubwa ya kuzaa mtoto tahira au aliyepumbaa. Wasia wa nne: usifanye tendo la ndoa kisha ukaacha bila ya kutokwa na manii, na endapo utadumu na tabia hii una hatihati ya kupata vijiwe katika kibofu. Wasia wa tano: epuka sana tabia ya uvivu na hali ya kujaza sana tumbo chakula pamoja na vinywaji. Wasia wa sita: matabia husema, " mtu anywe maji anapokuwa na kiu, na ajinyooshe (apumzike) baada ya kula chakula cha mchana, na atembee baada ya kula chakula cha usiku, asilale bila ya kwenda chooni, ajihadhari kuoga baada ya kula akashiba na kujamiiana na mwanamke mzee hutia maradhi mwenye afya. Wasia wa saba: amesema tabibu mmoja kuwa " mambo manne yanadhuru kiwiliwili, jimai ikiwa tumbo limejaa (umeshiba), kuoga ikiwa umeshiba, kula nyama iliyokaushwa juani na kujamiiana na vizee. Wasia wa nane: walikusanyika watu kwa tabibu mmoja ambaye alikuwa anakaribia kufa, watu wale walitaka wapate wasia wa afya kutoka kwake. Tabibu yule akawausia kuwa "msile tunda mpaka liwe limeiva, akila mtu chakula chake cha mchana basi alale kidogo tu, na asilale mtu baada ya kula chakula cha usiku mpaka atembee kidogo hata kama ni hatua arobaini.” Wasia wa tisa: mfalme mmoja alimwambia tabibu wake, "Nisifie sifa ambazo nitajifunza kutoka kwako” tabibu akamwambia: " Usile dawa isipokuwa kwa ugonjwa, usile tunda ila bivu, wala usimeze chakula mpaka uwe umekitafuna sana na kuwa laini, ukila mchana lala kidogo, ukila usiku ussilale mpaka utembee walau hatua hamsini, wala usile mpaka uwe una njaa, wala usizuie mkojo, wala usile chakula hali ya kuwa ndani ya tumbo tayari kuna chakula yaani umeshiba (kula ukiwa na njaa), usile kile ambacho meno yako hayawezi kutafuna kwani hakitaweza kumeng’enywa tumboni, na kitu chenye thamani kubwa sana katika mwili wako ni ile damu yako, basi usiitoe mpaka kuwe na haja ya dharura ya kuitoa.” Wasia wa kumi: tabibu mmoja alisema "mambo manne hudhoofisha mwili, kuzidisha kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, kuwa na hamu nyingi, kunywa maji mengi kabla ya kula, na kula vitu vikali.” Wasia wa kumi na moja: mambo mawili hutia nguvu kiwiliwili, 1. Kula chakula kitamu na kizuri, 2. Kunukia harufu nzuri. Huo ndio baadhi ya wasia wa matabibu mbalimbali katika kuboresha na kulinda afya ya mtu. Je kwa upande wako ni wasia upi umekuvutia? Au ni wasia upi hujauelewa kwa maelezo yake? Kuwa huru uliza lolote juu ya makala hii tupo pamoja kwaajili ya kudumisha jamii katika kulinda afya zetu. Napenda kuongezea kitu kimoja muhimu kabisa kwamba, vijana tuepuke sana kulala asubuhi kwani hali hii hutukosesha rizki na asubuhi ndio muda wa watu kutafuta rizki. Nakutakia kila la kheri ndani ya Staryte(The Informative) kwa kujifunza mambo mbalimbali. | |
Views: 1793 | | |
Total comments: 0 | |