Home » Articles » HEALTH |
Nini maana ya Kufeli au kufa kwa moyo? (Heart failure) Na nini kisababishi? Ingawa inaweza kuleta maana hiyo Lakini kufa kwa moyo haina maana kwamba moyo umeshindwa kufanya kazi au umefeli. Kufeli kwa moyo ni hali mbaya sana ambayo moyo hausukumi damu ipasavyo katika mwili. Upande wa kulia wa mgonjwa au kushoto au hata kotekote kunaweza kuathirika. Dalili zake hutegemea ni upande upi umeathirika na ni kwa kiasi gani kufeli kwa moyo kumejitokeza. Kutokana na baadhi ya wataalamu wa mambo ya moyo wameweza kueleza kwamba kufeli kwa moyo ni "ukosefu wa kazi hii ya kusuma damu vizuri katika mwili, hivyo pampu zinashindwa kuzungusha damu mwilini na matokeo yake kuw ana msongamano mkubwa sana katika tishu (tissue).
Kuna aina kama tatu hivi za matatizo ya moyo ambayo watu wengi sasa huchanganya au hushindwa kutofautisha, nayo ni Heart Failure, Heart Attach na Cardiac Arrest. Hebu tuangalie tofauti za matatizo haya.
Kwa kufupisha ni kwamba Heart attack ina maana seli za moyo hufa kutokana na kukosa oxygen, Heart failure ina maana moyo hausukumi damu ipasavyo na Cardiac arrest ni moyo kusimama kabisa. Je, nini alama au daliliza tatizo hili? (Heart Failure) Unashauriwa kumuona mtaalamu wa moyo haraka sana endapo utaona una dalili hizi.
Dalili zingine hutegemea ni upande gani umeathirika
1. Upungufu wa pumzi, kutweta – hii huweza kutokea muda wowote, Lakini huweza kugundulika kwa urahisi zaidi endapo mgonjwa atakuwa amelala au kujishughulisha. Mgonjwa usiku atakuwa anahitaji kukaa badala ya kulala ili apate hewa nyingi iliyo safi. 2. Kukohoa 3. Kutoa mapovu wakati wa kukohoa Hii hutokea pale damu inaporudi katika vena za pulmonary, kwasababu moyo umeshindwa kuendelea kusukuma damu hivyo kusababisha kimiminika kuingia katika mapafu
1. Kuvimba kwa visukusuku vya miguu na mikono 2. Kuvimba miguu 3. Kutanuka kwa ini 4. Kuvimba tumbo Hali hii hutokea pale damu inapotoka kwenye moyo inapopungua kasi, hivyo damu inayorudi katika moyo kupitia mishipa hurudi, na kusababisha kujaa kwa kimiminika katika tishu. Figo hupata shida sana kuchuja maji na chumvi ambayo husababisha upungufu wa kimiminika katika tishu.
1. Kizunguzungu – jinsi kiasi cha sodium na vitu vingine katika damu vinapobadilika ndipo mgonjwa hupata uwezekano mkubwa sana wa kuhisi kizunguzungu na kuchanganyikiwa. 2. Kichefuchefu 3. Kufunga choo (constipation) 4. Kukosa hamu ya kula – pindi mfumo wa mmeng’enyo unapopokea damu chache, ndipo mgonjwa huhisi kukosa hamu ya kula na matatizo ya mfumo wa mmeng’enyo. Tumeona dalili za kufahamu kama una tatizo la kufeli kwa moyo sasa hebu tuangalie ni vitu gani ambavyo vinavyosababisha tatizo hili? Zifuatazo ndiyo sababu:
· Hyperthyroidism (kupitiliza au kuzidi kwa tezi za thyroid).
· Hypothyroidism (kupunguza kwa tezi za thyroid).
· Kufeli kwa moyo upande wa kushoto kunaweza kusababisha kufeli upande wa kulia.
· Kuharibika kwa valvu za moyo.
Kwa upande wangu nina hayo tu, ikiwa una la ziada itakuwa ni bora tukachangia mada kwa lengo la kuelimisha jamii na kutatua matatizo. Jisikie huru katika mtandao huu wa Staryte – The informative where we get what we find. Ahsante. | |
Views: 3115 | |
Total comments: 0 | |